Sasa Unaweza Ku-edit Comment Kwenye Instagram 1

Sasa Unaweza Ku-edit Comment Kwenye Instagram

Utaweza ku-edit maoni yako ndani ya dakika 15 tu toka ulipo chapisha

Instagram imetangaza kipengele kipya ambacho hatimaye kinawaruhusu watumiaji wa mtandao huo kuhariri (Edit) maoni baada ya kuchapisha, kukiwa na angalizo kwamba watumiaji wana muda wa dakika 15 pekee kufanya hivyo.

Sharti jingine ni kwamba unaweza tu kuhariri maandishi kwenye maoni, kwa mfano, ikiwa maoni yana maandishi na picha za gif au nyingine, unaweza tu kuhariri maandishi pekee.

Sasa Unaweza Ku-edit Comment Kwenye Instagram 2

Hata hivyo, hakuna kikomo cha idadi ya mara unazo weza kuhariri maoni kwenye Instagram ndani ya dakika 15 baada ya kuyachapisha.

Pamoja na hayo ni vyema kutambua kwamba mara maoni yanapohaririwa, watumiaji wengine wa Instagram watajua kuwa yamehaririwa, kwani lebo ya “Imehaririwa” (Edited) itaonyeshwa kwenye maoni hayo. Hata hivyo, hawataweza kuona historia ya mabadiliko yaliyofanywa.

Previous Post
Claude Mythos Toleo Jipya la AI Lenye Kutishia Usalama 3
Claude Mythos Toleo Jipya la AI Lenye Kutishia Usalama