in

Weka Password Kwenye File Bila kutumia Programu

Weka Nywila au Password kwenye Folder lolote kwenye kompyuta yako

Password4:46

Kuna njia nyingi sana za kuweka password au (nywila) kwenye Folder na File za kompyuta yako, lakini njia hizo nyingi ni lazima kutumia programu maalum ambayo ndio husaidia kuweka ulinzi wa password kwenye file au folder lako kwenye kompyuta yako.

Mara nyingi njia hizi si salama kwani pale mtu anapofuta programu hiyo kwenye kompyuta yako ina maana pia ma-file na mafolder yako yatakua haya tena ulinzi maalum wa password.

Ifuatayo ni njia rahisi na salama ya kuweka password (nywila) kwenye mafolder ya kompyuta yako bila kutumia programu yoyote, kwa kuanza basi unahitaji kuwa na kompyuta inayotumia Windows kuanzia Windows xp na kuendelea na pia hakikisha kwenye kompyuta yako inayo programu ya Notepad ambayo mara nyingi inakwepo ndani ya kompyuta yako baada ya hapo fuata maelekezo haya.

Hatua ya kwanza nenda mpaka hapo chini mwisho kabisa wa code upande wa kulia kwenye kona palipo andikwa view raw kisha bofya hapo na copy code zinazo-onekana.

Aina Tatu za Telegram Bots Bora, Jaribu Kupitia Telegram

Copy Code Hapa

Kisha fungua Notepad alafua paste Code hizo ulizo copy awali, kisha kwenye code hizo tafuta sehemu hii “NOT %pass%== 887872zd goto FAIL” kisha badilisha namba hizi 887872zd kuwa password unayotaka kisha Save file hili kwa jina la Folderlock.bat pia hakikisha mahali palipo andikwa “save as type” pamekuwa kwenye sehemu ya “All Files” kisha save file lako kwenye sehemu unapotaka kuhifadhi folder lako lenye nywila au password.

Baada ya hapo nenda ulipo hifadhi file lako la Folderlock.bat kisha bofya mara mbili kwenye file hilo, kwa kufanya hivyo utaona folder lenye jina la MyFolder limetoke chukua vitu onavyotaka kuvifunga na password kisha viweke ndani ya folder hilo la MyFolder.

Kisha bofya tena mara mbili file la Folderlock.bat kisha utaona maandishi yakiwa yanakuuliza kama unataka kufunga file lako kisha andika Y kwenye keyboard yako kisha bofya Enter hapo utaona folder la MyFolder limepotea.

Baada ya kufanya hivyo utakuwa umeweza kuweka password kwenye folder lako bila kutumia programu yoyote, ili kuangalia folder lako bofya mara mbili file la Folderlock.bat kisha weka password yako iliyoiandika awali kisha bofya Enter na utaona folder lako limetokea tena, kulifunga fuata njia za awali bofya mara mbili folder la Folderlock.bat kisha andika Y kisha bofya Enter folder lako litapotea.

Zuia Bando Kuisha Unapo Angalia Video Kupitia YouTube

Bila shaka mpaka hapo utakua umeweza kuweka password kwenye folder lako bila kutumia programu yoyote kama unataka kujufunza mafunzo mengine mbalimbali endelea kutembelea blog ya tanzania tech kila siku au unaweza kupata habari zote za teknolojia moja kwa moja kwenye simu yako ya mkononi kwa ku-download App ya Tanzania tech  moja kwa moja kwenye simu yako ya Android, pia unaweza kujiunga nasi kwa barua pepe pamoja na mitandao yetu ya kijamii ya Facebook, Twitter, Instagram pamoja na Yotube kwa kujifunza mambo mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video.

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

16 Comments