in

Jinsi ya Kudivert SMS Kwenda Simu Nyingine Ndani ya DK 1

Jifunze hapa njia nyingine ya kuforwad meseji kutoka simu moja kwenda nyingine

Jinsi ya Kudivert SMS Kwenda Simu Nyingine Ndani ya DK 1

Kama wewe ni msomaji wa Tanzania Tech basi lazima unajua kuwa tulishawahi kuzungumzia njia ya kuforward SMS kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine. Kama bado hufahamu kuhusu njia hiyo unaweza kusoma hapa kujua hatua kwa hatua.

Lakini baada ya kuonyesha njia hiyo watu wengi walisema kuwa njia hiyo inakuja na mambo mengi na pengine inaweza kumshinda mtu asiye na ujuzi wa kutumia simu ya Android.

Kuliona hilo hivi leo nimekuletea njia nyingine ambayo ni rahisi zaidi ambayo itakusaidia ku forward meseji kutoka namba moja ya simu kwenda namba nyingine. Kumbuka njia hii inaweza kufanya kazi kwa watumiaji wa simu za Android 5.0 na kuendelea. Kama unatumia Android 4.0 basi endelea kutembelea Tanzania Tech tutaleta njia hii kupitia mfumo huo siku za karibuni.

Basi baada ya kusema hayo moja kwa moja twende kwenye hatua hizi rahisi na fupi. Kwa kuanza hakikisha una download app ya SMS Forward kupitia link hapo chini. App hii haipatikani kupitia soko la Play Store hivyo hakikisha unapakua kupitia link hapo chini.

Fahamu eSIM Mfumo Mpya wa Laini za Simu za Kidigitali

Download App ya SMS Forward

Baada ya kudownload na ku-install vizuri app hii sasa unaweza kuendelea kwa kufanya setup hizi rahisi. Baada ya kufungua app hii bofya sehemu ya jumlisha iliyopo chini upande wa kulia.

Jinsi ya Kudivert SMS Kwenda Simu Nyingine Ndani ya DK 1

Baada ya hapo utaletewa ukurasa ambapo unatakiwa kuchagua namba ambayo meseji zikitumwa kwenye namba hiyo basi moja kwa moja ziweze kupelekwa kwenye namba nyingine. Bofya hapo na chagua namba hiyo kupitia kwenye phonebook ya simu yako.

Jinsi ya Kudivert SMS Kwenda Simu Nyingine Ndani ya DK 1

Baada ya hapo utarudishwa tena kwenye ukurasa huu na kisha chagua tena sehemu ya mstari wa chini yake na chagua namba ambayo itakuwa inapokea meseji zote zitakazo kuwa zinatumwa kwenye namba uliyo chagua kwenye hatua ya awali.

Jinsi ya Kudivert SMS Kwenda Simu Nyingine Ndani ya DK 1

Baada ya kuchagua namba zote yaani ya mpokeaji wa meseji na namba ambayo unataka ku-forward meseji zake moja kwa moja sasa bofya sehemu ya Add iliyopo chini katika.

Jinsi ya Kudivert SMS Kwenda Simu Nyingine Ndani ya DK 1

Baada ya hapo sasa unaweza kuwezesha meseji ziweze ku-forwardiwa kwa kuwasha sehemu ya Switch kama inavyo onekana kwenye picha hapo chini.

Fahamu Haya Kwenye Processor Kabla ya Kununua Laptop

Jinsi ya Kudivert SMS Kwenda Simu Nyingine Ndani ya DK 1

Baada ya hapo basi moja kwa moja kila meseji ambayo namba ya mwanzo itakuwa inapokea basi moja kwa moja utakuwa unaweza kupata kupitia namba ya pili. Kitu cha muhimu ni kuhakikisha simu inayo pokea meseji inayo SMS au muda wa maongezi kwa ajili ya kutuma SMS hiyo kwenye namba ya pili.

Kama unataka njia yenye uwezo wa kufanya mambo mengi zaidi basi unaweza kuangalia njia ya kwanza ambayo inakupa uwezo wa kupokea meseji kutoka kwenye kundi la watu au hata mtu mmoja mmoja, pia unaweza ku-forward meseji za watu ambao hata awapo kwenye phonebook yako ikiwa na mambo mengine.

Kama kuna mahali umekwama unaweza kutuandikia kupitia sehemu ya maoni hapo chini. Kama unataka kujifunza zaidi hakikisha una soma hapa jinsi ya kupokea SMS kupitia app ya Telegram.

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

5 Comments