in

Ongeza Ukubwa, Ngarisha Picha Bila Kupoteza Ubora (Android)

Utaweza kungarisha picha na kuongeza ukubwa wa picha mara 100 zaidi

Ongeza Ukubwa, Ngarisha Picha Bila Kupoteza Ubora (Android)

Ni mara nyingi sana imekuwa ni kawaida watu kutumia picha ambazo hazina ubora, hii inatokana na kudownload picha hizo kutoka kwenye vyanzo ambavyo hubadilisha picha na kuwa na size ndogo na pamoja na quality mbaya.

Kuliona hili leo nimekusogezea njia hii rahisi sana ambayo inaweza kusaidia sana kuweza kuongeza ukubwa wa picha, ikiwa pamoja na kuongeza ubora au kungarisha picha kwa asilimia kubwa sana.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Njia hii inatumia mfumo au teknolojia ya AI kuweza kungarisha rangi pamoja na kukuza picha bila picha hiyo kupoteza ubora wake. Kama unavyoweza kuona kwenye picha hapo chini.

Ongeza Ukubwa, Ngarisha Picha Bila Kupoteza Ubora (Android)

Mbali ya kuongeza ukubwa wa picha, njia hii inaweza kutakatisha picha hata kama picha hiyo haionekani vizuri na kufanya rangi ziweze kungaa na picha iweze kuonekana vizuri.

Ongeza Ukubwa, Ngarisha Picha Bila Kupoteza Ubora (Android)

Kwa kuanza unachotakiwa kufanya ni kudownload app hapo chini, baada ya kudownload app hapo chini sasa endelea kwenye hatua ambazo nime kuonyesha.

Download App Hapa

Kwa kuanza fungua app hii kisha chagua kitu ambacho unataka kufanya, app hii inaweza kukusaidia kufanya mambo mbalimbali na unaweza kuchagua kwa kubofya sehemu ya menu kwa juu.

Ongeza Ukubwa, Ngarisha Picha Bila Kupoteza Ubora (Android)

Unaweza kuchagua kupitia sehemu ya Enlarge ambayo itakusaidia kuongeza ukubwa wa picha, sehemu ya Enhance hii itarekebisha rangi kwenye picha, na sehemu ya sharpen itangarisha picha, na sehemu ya reduce noise hii itaondoa sehemu ambazo hazionekana vizuri kwenye picha na kuzifanya zionekane vizuri.

Ongeza Ukubwa, Ngarisha Picha Bila Kupoteza Ubora (Android)

Baada ya hapo bofya sehemu ya picha katikati ili kuchagua picha kwenye simu yako. Hakikisha unabofya sehemu ya picha iliyochowa katikati kwenye app hii.

Ongeza Ukubwa, Ngarisha Picha Bila Kupoteza Ubora (Android)

Baada ya hapo bofya sehemu ya Upload iliyopo chini mwisho kabisa na moja kwa moja subiri na baada ya muda utaweza kuona picha yako imerekebishwa vizuri.

Ongeza Ukubwa, Ngarisha Picha Bila Kupoteza Ubora (Android)

Kwa kuwa njia hii inatumia teknolojia ya AI inafanya kazi kwa kuangalia aina ya rangi zilizopo kwenye picha hivyo ni wazi kuwa sio kila picha inaweza kubadilisha kwa asilimia 100. Kitu cha msingi jaribu njia hii kwenye picha tofauti kuweza kupata matokeo bora zaidi.

Kwa kufanya hatua hizo natumaini utakuwa umeweza kuongeza ukubwa na kungarisha picha zako kwa urahisi kupitia simu yako ya Android bila kupoteza ubora wake. Kama unataka kujifunza zaidi unaweza kusoma hapa kujua jinsi ya kuweka alama au watermark kwenye picha zako kwa urahisi kupitia simu yako ya Android.

Ongeza Ukubwa, Ngarisha Picha Bila Kupoteza Ubora (Android)
Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Jinsi ya Kufuta kwa Haraka Majina Yaliyo Jirudia

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

4 Comments