in

Jinsi ya Kujiweka kwenye Google Search Kama Mtu Maarufu

Mtu akitafuta jina lako utaweza kuonekana kama ilivyo kwa watu maarufu kupitia Google

Jinsi ya Kujiweka kwenye Google Search Kama Mtu Maarufu

Katika ulimwengu huu wa sasa ni wazi kuwa mambo mengi sana yanaenda kidigital, siku hizi imekuwa ni muhimu sana kwa mtu yoyote kuweza kuwa na wasifu mzuri mtandaoni kwani hii inaweza kusaidia wewe kufanikiwa kwenye mambo mbalimbali ya muhimu.

Kuliona hili leo nimekuletea njia mpya na rahisi ambayo unaweza kutumia kuweza kuweka jina lako kwenye mtandao wa Google ili pale mtu anapo tafuta jina lako, basi moja kwa moja jina lako liweze kuonekana na wasifu wako kama inavyo kuwa kwa watu mbalimbali maarufu.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Jinsi ya Kujiweka kwenye Google Search Kama Mtu Maarufu

Kabla ya kuanza hatua hizi ni vyema kujua kuwa unahitaji kuwa na app ya Google search kwenye simu yako, au browser ya Google Chrome kwenye simu yako. Pia ni muhimu kufahamu kuwa njia hii inawezekana endepo unatumia simu yako ya mkononi na sio kompyuta.

Kama tayari unayo mahitaji yote hayo sasa moja kwa moja twende kwenye hatua kwa hatua jinsi ya kuweka jina lako kwenye mtandao wa Google.

Kwa kuanza ingia kwenye Google Chrome kisha andika jina lako kamili kwenye sehemu ya kutafuta na kisha bofya kitufe cha kutafuta, baada ya hapo shuka chini kabisa mwisho wa ukurasa huo, chagua lugha ya Kingereza au English kama simu yako ipo kwenye lugha ya Kiswahili

Jinsi ya Kujiweka kwenye Google Search Kama Mtu Maarufu

Baada ya kuchagua English moja kwa moja bofya kitufe cha More kinacho onekana mwisho kabisa pembeni ya sehemu ya lugha.

Jinsi ya Kujiweka kwenye Google Search Kama Mtu Maarufu

Baada ya kubofya hapo moja kwa moja utapelekwa kwenye uwanja wa settings kupitia kivinjari cha Chrome, kupitia ukurasa huo tafuta maandishi yaliyo andikwa “Region for Search Results“.

Jinsi ya Kujiweka kwenye Google Search Kama Mtu Maarufu

Chini yake utaweza kuona “Tanzania”, bofya hapo na utaweza kuona list ya nchi mbalimbali na moja kwa moja chagua “Kenya“.

Jinsi ya Kujiweka kwenye Google Search Kama Mtu Maarufu

Baada ya hapo shuka mwisho wa ukurasa huo na bofya kitufe cha Save. Baada ya kusave malizia kwa kubofya OK kwenye maandishi yanayotokea.

Jinsi ya Kujiweka kwenye Google Search Kama Mtu Maarufu

Mara baada ya kubofya OK utaweza kurudishwa kwenye matokeo ya Jina lako na sasa utaweza kuona sehemu mpya ambayo imeandikwa “Add yourself to Google Search” bofya kitufe cha “Get Started” kinacho onekana upande wa kulia juu kabisa.

Jinsi ya Kujiweka kwenye Google Search Kama Mtu Maarufu

Baada ya kubofya hapo moja kwa moja utafunguka ukurasa maalum, lakini kabla ya kuendelea utatakiwa kuthibitisha namba yako ya simu, kumbuka namba hii iitakuwa kama uthibitsho maalum wa ukurasa wako kupitia Google.

Jinsi ya Kujiweka kwenye Google Search Kama Mtu Maarufu

Chagua nchi ya Tanzania kwenye alama ya bendera kisha malizia kwa kuweka namba yako ya simu, moja kwa moja utatumiwa kodi maalum ambayo utaiweka kwenye sehemu zilizoko wazi baada ya kubofya kitufe cha Next chini ya ukurasa huo.

Jinsi ya Kujiweka kwenye Google Search Kama Mtu Maarufu

Baada ya kuokea uthibitisho sasa utaweza kuanza kujaza fomu hiyo maalum ambayo vitu hivyo ndivyo vitakuwa vinaonekana pale watu watakapo tafuta jina lako kupitia Google.

Jinsi ya Kujiweka kwenye Google Search Kama Mtu Maarufu

Hatua zote zilizo wekewa alama ya nyota ni hatua za muhimu hivyo hakikisha unajaza hatua hizo kwa usahihi bila kuruka hata hatua moja, hatua hizo zipo nne kuanzia juu ambazo ni Name au Jina lako ambalo litakuwa limejijaza tayari, Location au mahali ulipo, na maelezo kuhusu wewe au About, bila kusahau sehemu ya Occupation au kazi yako.

Baada ya hapo sehemu nyingine unaweza kuzijaza kwa mapendekezo yako na kama unataka zionekane kwenye Google.

Baada ya kujaza sehemu zote ikiwa na sehemu za mitandao ya kijamii moja kwa moja bofya Preview kuona muonekano wa ukurasa wako.

Jinsi ya Kujiweka kwenye Google Search Kama Mtu Maarufu

Kama umerithika na kila kitu basi moja kwa moja bofya sehemu ya Save ambayo inapatikana chini kwenye ukurasa huo baada ya kubofya preview.

Jinsi ya Kujiweka kwenye Google Search Kama Mtu Maarufu

Baada ya hapo bofya sehemu ya “View search card” inayotokea mara baada ya ku-save maelezo yako yote. Baada ya hapo utapelekwa kwenye Google search na utaweza kuona jina lako limetokea kwenye matokeo pale mtu atakapo tafuta jina lako.

Jinsi ya Kujiweka kwenye Google Search Kama Mtu Maarufu

Baada ya kufanya hatua zote hizo moja kwa moja utakuwa umeweza kuweka profile yako kwenye mtandao wa Google na kuonekana kama inavyo onekana kwa watu mbalimbali maarufu.

Jinsi ya Kujiweka kwenye Google Search Kama Mtu Maarufu

Kitu cha muhimu kufahamu ni kuwa, kwa sasa sehemu hii inapatikana kwa watumiaji wa lugha ya kiingereza tu na Google wametangaza kuwa sehemu hii sasa inapatikana nchini Kenya, Nigeria na Afrika ya kusini, huku ikitegemewa kuja Tanzania na nchi nyingine siku za karibuni.

Kwa sasa njia hizo hapo juu ndizo zitakazo kusaidia kupata profile yako kupitia Google kama watu maarufu mbalimbali. Kumbuka pia Google imedai kuwa profile yako inaweza isionekana kutokana na wasifu wako hivyo nadhani hii sio ya kila mtu. Nadhani kama wewe ni mtu muhimu au public figure au una nyazfa fulani muhimu basi hii inaweza kuwa muhimu sana kwako.

Kama unataka kujua zaidi kuhusu sehemu hii unaweza kusoma hapa kujua zaidi kupitia tovuti ya Google Africa.

Jinsi ya Kujiweka kwenye Google Search Kama Mtu Maarufu
Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Jinsi ya Kupata File Lolote kwa Haraka (MP3,MP4,ZIP,PDF,ISO)

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

2 Comments