in

Apps za Kusaidia Kutumia Simu ya Mtu Kwenye Simu Yako

App za kusaidia Kutumia simu mbili za Android kwenye simu moja

Apps za Kusaidia Kutumia Simu ya Mtu Kwenye Simu Yako

Kuna wakati unakuta unataka kumsaidia mtu kufanya kitu fulani kwenye simu yake na unakuta uko mbali nae, iwe unataka kumsaidia rafiki, ndugu ama jamaa app hizi nzuri zinaweza kukusaidia sana kuunganisha simu yako na simu ya unayetaka kumsaidia kitu hicho.

Kabla ya kuanza kuzitaja app hizi labda nikueleze tena kwa undani kidogo jinsi app hizi zinavyofanya kazi.

App hizi zinakusaidia kuweza kuunganisha simu yako na ya mtu mwingine huku ukipata uwezo wa kutumia simu ya mtu huyo kupitia kwenye simu yako, yaani kwa kifupi apps hizi ni kama vile (remote control) lakini hii inakupa uwezo wa kuona kila kitu anacho weza kuona mtu kwenye simu nyingine, yaani ni sawa na kutumia simu ya mtu kwenye simu yako, kunielewa zaidi angalia video hapo chini.

Basi baada ya kuangalia video hiyo natumaini utakuwa umejua kazi ya apps hizi, basi moja kwa moja twende tukangalie apps hizi nzuri za Android. Kumbuka unaweza kudownload apps hizi kwa kubofya jina la app husika.

Download App Hapa

Inkwire ni app nzuri sana ya android ambayo itakuwezesha kuunganisha simu moja na nyingine, app hii ni rahisi kutumia na unaweza kuunganisha simu kwa kutumia namba maalum za Access code ambazo unashare na mtu mwingine mwenye app hii na moja kwa moja utaweza kutumia simu ya mtu mwingine kwenye simu yako.

Mbadala wa (IDM) Download Kwa Haraka Kwenye Kompyuta

Download App Hapa

TeamViewer QuickSupport ni app nyingine nzuri ambayo inaweza kukusaidia sana kuweza kunganisha simu mbili kwa wakati mmoja. App hii ni maarufu sana kwenye upande wa kompyuta na pia sasa inapatikana kwenye mfumo wa Android na ni rahisi sana kutumia. Uzuri wa app hii ni kuwa unaweza kuendesha simu yoyote sio android pekee yaani iwe iOS au Android app hii inaweza kuunganisha simu zote.

Download App Hapa

Join me ni application nyingine nzuri sana ya Android inayoweza kuunganisha simu mbili, uzuri wa app hii ni kuwa unachotakiwa kufanya ni kushare link kutoka simu moja kwenda kwenye simu nyingine na moja kwa moja utaweza kutumia simu ya mtu kwenye simu yako ya Android. Kitu kingine kizuri kuhusu app hii ni kuwa inakuja na uwezo wa LIve chat hivyo unaweza kumsaidia mtu kitu huku mnasikilizana.

RemoDroid
Price: Free

Download App Hapa

Remo droid ni app nyingine nzuri ya kuunganisha simu za Android, utofauti uliopo kwenye app hii ni kuwa unaweza kuunganisha screen na simu nyingine iwapo tu simu zenu zote zimeunganishwa kwenye mtandao mmoja yani kama vile WiFi.

Ongeza Ulinzi Kwenye Simu ya Android kwa Njia Hizi

Download App Hapa

Miracast ni app nyingine ambayo itakusaidia kuunganisha simu za Android na pia itakusaidia kuunganisha simu yako na Smart TV yako. Pia mbali na TV kwa kutumia app hii unaweza kuunganisha simu yako na kifaa chochote chenye kioo pamoja na uwezo wa kupokea mtandao kwa kutumia wireless.

Download App Hapa

AirMirror ni app nyingine nzuri ya Android ambayo itakusaidia kuunganisha simu moja na nyingine, app hii ni nzuri kwa sababu inakusaidia kuunganisha simu zaidi ya mbili na pia utakuwa na uwezo wa kubadilisha simu inayo endesha nyenzake kwa kubofya kitufe kimoja tu.

Na hizo ndio app nzuri ambazo zinaweza kusaidia kuunganisha simu moja na nyingine, kumbuka apps hizi zote zinapatiikana Play Store hivyo hakikisha una download app hizi kuweza kuona jinsi zinavyofanya kazi. Kama kuna mahali utakwama jinsi ya kuweza kutumia apps hizi unaweza kuuliza kupitia sehemu ya maoni hapo chini.

Kama unataka kujua apps nyingine nzuri za android unaweza kusoma hapa kuweza kujua app nzuri zinazoweza kusaidia sana wanafunzi wote, iwe ni wanafunzi wa chuo au wanafunzi wa shule za sekondari apps hizo ni nzuri sana, ni vyema kusoma makala hizo kama wewe ni mwanafunzi.

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

One Comment