in

Apps Zinazoweza Kukusaidia Kutengeneza Pesa Mtandaoni

Njia za kutengeneza pesa mtandaoni kupitia Apps mbalimbali

Apps Zinazoweza Kukusaidia Kutengeneza Pesa Mtandaoni

Ukweli ni kwamba zipo njia nyingi sana za kutengeneza pesa mtandaoni, lakini sio kila njia ni rahisi na inalipa kweli, kupitia makala hii nitakuonyesha apps ambazo unaweza kutumia kutengeneza pesa mtandaoni moja kwa moja kupitia simu yako ya Android.

Kitu cha muhimu ni kuwa hakikisha unafanya kila ambacho nimekwambia kupitia app husika ili kuhakikisha unatengeneza pesa mtandaoni. Pia kumbuka kuwa sio kila app iliyopo hapa nimeijaribu kwa asilimia 100 hivyo ni vyema kuchukua muda wako kujaribu app zote ili kuona ni ipi inayolipa zaidi. Basi baada ya kusema hayo moja kwa moja twende kwenye makala hii

Apps Zinazoweza Kukusaidia Kutengeneza Pesa Mtandaoni

Kama wewe ni mmoja wa watu ambao wanapenda kupiga picha, na unauwezo wa kupiga picha nzuri basi app hii itakusaidia sana kutengeneza pesa mtandaoni.

Kupitia app hii utaweza kutengeneza pesa kwa kuuza picha zako kwa watu kwa urahisi, unachotakiwa ni kupakua app hii kisha tengeneza na thibitisha akaunti yako kisha anza kuweka picha zako ambazo uko tayari kuziuza, pia kama wewe ni model app hii pia inaweza kukusaidia sana picha zako kutumika.

Download App Hapa

Apps Zinazoweza Kukusaidia Kutengeneza Pesa Mtandaoni

Kama wewe ni mtumiaji wa mitandao ya kijamii kama Instagram, Twitter na mitandao mingine kama hiyo basi lazima utaipenda app hii. App hii ni mtandao wa kijamii ambao unakulipa kutumia mtandao huu, tofauti na mitandao mingine mtandao huu unakulipa kwa kila kitu unacho kifanya kwenye app hiyo ikiwa pamoja na kutengeneza akaunti.

Jinsi ya Kutengeneza Dollar $3 au $5 Mtandaoni (Njia Rahisi)

Mapato unayo yapata yanagawanywa kati yako wewe mtumiaji na wamiliki wa mtandao huo, mgawanyo huo ni wa asilimia 50 kwa 50. Kama unapenda mitandao ya kijamii basi pengine huu ni wakati wako wa kutengeneza pesa mtandaoni huku ukifurahia kufanya kitu unacho kipenda. Unaweza kupakua app hapo chini.

Download App Hapa

Apps Zinazoweza Kukusaidia Kutengeneza Pesa Mtandaoni

Kama wewe ni mmoja wa watu ambao wanapenda kuangalia video mtandaoni basi utaipenda app hii, app hii inakupa uwezo wa kutengeneza pesa huku ukiangalia video mbalimbali mtandaoni ikiwa pamoja na kufanya mambo mbalimbali.

Pia unaweza kutengeneza pesa kwa kualika watu kwenye app hii, app hii nimejaribu kuitumia hadi sasa nimepata coin 739 ambazo ni sawa na TZS 21.75. Unaweza kupakua app hii kupitia hapo chini pia kumbuka kuwa unaweza kualika watu ili kupata coin za bure kwa urahisi zaidi.

Download App Hapa

Apps Zinazoweza Kukusaidia Kutengeneza Pesa Mtandaoni

Kama umependa app ya kwanza kwenye list hii basi unaweza kuipenda pia app hii, tofauti na app ya kwanza ambayo utaweza kuuza picha moja kwa moja. App hii yenyewe ni mtandao wa kijamii ambapo watumiaji huweza kuuza picha zao moja kwa moja ikiwa pamoja na picha hizo kuingia kwenye mashindano ambayo picha itakayo shinda upata pesa zaidi.

Jinsi ya Kupata FREE Hosting Mwaka Mzima (Bure 100%)

App hii ni rahisi kutumia na unatakiwa kuendelea kutumia app hii kama ilivyo mtandao wa kijamii na utaweza kuona ukipata pesa moja kwa moja kwa moja kutoka kwenye app hii.

Download App Hapa

Apps Zinazoweza Kukusaidia Kutengeneza Pesa Mtandaoni

App ya mwisho kwenye list hii ni app ambayo itakulipa kufanya kazi mbalimbali mtandaoni, app hii itaweza kukulipa kwa kupiga picha, kujibu maswali na kufanya kazi mbalimbali. App hii ni rahisi kutumia na inaweza kukusaidia kutengeneza pesa mtandaoni kwa urahisi.

Kumbuka ni muhimu kukamisha kazi zote hadi mwisho ili kuweza kupata kiasi cha pesa kilicho ahidiwa kwenye kila kazi. Unaweza kupakua app hii kupitia link hapo chini.

Download App Hapa

Na hizo ndio apps ambazo zinaweza kukusaidia kupata pesa mtandaoni kwa sasa, kumbuka list hii inaweza kuendela hivyo hakikisha unapitia makala hii kila siku unapo pata nafasi. Kama unataka kujua njia nyingine za kutegeneza pesa mtandaoni unaweza kusoma hapa jinsi ya kutengeneza pesa kupitia app ya Telegram. Kwa maujanja zaidi hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania tech kila siku.

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

4 Comments