in

Kuondoa Beat Kwenye Nyimbo Yoyote (Tengeneza Acapella)

Jinsi ya kutengeneza Acapella ya nyimbo yoyote kwa haraka na urahisi

Kuondoa Beat Kwenye Nyimbo Yoyote (Tengeneza Acapella)

Kama wewe ni mfuatiliaji wa tovuti ya Tanzania Tech basi lazima utakuwa unajua hivi karibuni tulijifunza jinsi ya kuondoa maneno kwenye nyimbo yoyote na kubakiwa na beat. Lakini swali linabaki, inakuaje kama unataka kuondoa beat kwenye nyimbo yoyote na kubakiwa na maneno tu au acapella.

Njia hii ni rahisi fupi na haraka hivyo sitaku potezea muda mwingi kusoma maandishi mengi sana, kifupi nataka usikilize kwanza nyimbo hapo chini kisha utajua kama njia hii inafanya kazi au vipi.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Baada ya hapo sasa twende moja kwa moja nikuonyeshe ni njia gani ambayo unaweza kutumia kuondoa beat kwenye nyimbo yoyote na kubakiwa na maneno au (Acapella). Kumbuka njia inahitaji uwe na internet kwenye kifaa chako na kama tayari unayo internet basi moja kwa moja endelea kwenye njia zinazofuata.

Hakikisha unafuata hatua kwa hatua njia zote kabla ya kuendelea. Kwa kuanza ingia kwenye tovuti ya kupitia link hapo chini.

Tembelea Tovuti Hapa

Baada ya hapo, moja kwa moja bofya sehemu iliyo andikwa Drop or click to upload your audio. Chagua nyimbo unayotaka kuondoa beat kisha bofya Open kuanza ku-upload.

Subiri kidogo na kisha utaruhusiwa kudownload nyimbo yako ikiwa hina beat…. rahisi ehh. Sikia hii nyimbo mpya ya Roma niliyo tumia njia hii kuondoa beat…

Mpaka hapo natumaini utakuwa umeweza kuondoa beat kwenye nyimbo yoyote ile unayotaka, kama unataka kuondoa maneno kwenye nyimbo yoyote basi unaweza kusoma makala yetu iliyopita.

Kuondoa Beat Kwenye Nyimbo Yoyote (Tengeneza Acapella)
Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Jinsi ya Kupata Namba za Simu za Zamani Ulizopoteza

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

2 Comments