in

Mkurugenzi Mtendaji wa Twitter Jack Dorsey Ajiuzulu

Mkurugenzi mpya wa Twitter kwa sasa ni Parag Agarwal

Mkurugenzi Mtendaji wa Twitter Jack Dorsey Ajiuzulu
Mkurugenzi Mtendaji wa Zamani wa Twitter Jack Dorsey

Habari kubwa siku ya leo, mkurugenzi mtendaji wa zamani wa Twitter Jack Dorsey, hivi leo ametangaza rasmi kuachia kiti chake cha ukurugenzi kwenye kampuni ya Twitter.

Kwa mujibu wa barua yake ya kujiuzulu, Jack Dorsey ametangaza kuwa ameamua kujiuzulu kwa mapenzi yake na uamuzi huu ni mgumu lakini ni uamuzi sahihi kwa wakati huu.

Jack Dorsey ni mmoja wa waanzilishi wa mtandao wa Twitter na alikuwa CEO au mkurugenzi mtendaji wa mtandao huo tokeo mwaka 2006, hadi hapo siku ya jana.

Kwa mujibu wa barua yake ya kujiuzulu, Jack Dorsey amemteua Parag Agarwal ambaye alikuwa CTO wa kampuni hiyo kuchukua nafasi yake ya CEO. Hata hivyo Jack Dorsey ataendelea kuwa kwenye bodi hadi hapo May 2022 na baada ya hapo ataondoka kabisa kwenye kampuni ya Twitter.

Mkurugenzi Mtendaji wa Twitter Jack Dorsey Ajiuzulu
Parag Agarwal Mkurugenzi Mtendaji Mpya wa Twitter

Moja ya sababu ambazo Jack amezitoa ni pamoja na kuamini kuwa Twitter inaweza kujiendesha na hakuna haja ya yeye kama mwanzilishi kuendelea kuongoza kampuni hiyo.

I believe it’s critical a company can stand on its own, free of its founder’s influence or direction,” alisema Jack Dorsey kwenye email yake ya kujiuzulu.

Hizi Hapa Tovuti Bora za Kupakua Movie Mpya (Bure)

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.