in

Mabadiliko ya Muhimu Kwenye Simu za iPhone 13 na 13 Mini

Hizi hapa simu mpya za iPhone 13 na iPhone 13 Mini

Mabadiliko ya Muhimu Kwenye Simu za iPhone 13 na 13 Mini

Hatimaye baada ya kuangalia uzinduzi wa iPhone 13 na bidhaa mpya za Apple hapo jana, sasa ni wakati wa kuongelea yote mapya kupitia uzinduzi huo.

Kupitia makala hii tutaenda kuangalia simu mpya za iPhone 13 na 13 Mini, mabadiliko muhimu kuhusu simu hizi, huku maswala ya sifa na bei unaweza kusoma moja kwa moja kupitia tovuti ya Price in Tanzania. Basi bila kupoteza muda twende moja kwa moja kwenye makala hii.

iPhone 13 na iPhone 13 Mini

Kwa mwaka huu (2021) kampuni ya Apple imezindua matoleo manne, iPhone 13, iPhone 13 Mini, iPhone 13 Pro pamoja na iPhone 13 Pro Max. Simu zote hizi zinakuja na sifa ambazo zimetofautiana kwa upande wa kioo, kamera pamoja na uhifadhi wa ndani.

Kwa upande wa iPhone 13 na iPhone 13 Mini pia zote zinakuja na tofauti hizi.

Kioo

Tukianza na kioo, iPhone 13 na iPhone 13 Mini zinakuja na vioo vyenye ukubwa tofauti huku iPhone 13 ikiwa inakuja na kioo kikubwa cha inch 6.1, na iPhone 13 mini ikiwa na kioo cha inch 5.4.

Mabadiliko ya Muhimu Kwenye Simu za iPhone 13 na 13 Mini

Mbali na hayo, simu zote mbili zinakuja na kioo cha Super Retina XDR OLED, kioo ambacho pia kinakuja na teknolojia ya HDR10 pamoja na Dolby Vision huku ikiwa na uwezo wa kuonyesha mwanga au nits hadi 800 (typ), na nits 1200 ikiwa (peak).

Kampuni ya TECNO Yazindua Rasmi Spark 10 PRO

Vioo hivi pia vime tengenezwa kwa glass yenye ulinzi wa kuzuia mikwaruzo au Scratch-resistant ceramic, pamoja na oleophobic coating.

Kamera

Mabadiliko ya Muhimu Kwenye Simu za iPhone 13 na 13 Mini

Kwa upande wa kamera, iPhone 13 na iPhone 13 Mini zinakuja na kamera mbili kwa nyuma ambazo zimekaa kwa mshazari tofauti na iPhone 12. Kamera zote za nyuma kwenye simu hizi mpya zinakuja na Megapixel 12 kila moja, huku zikiwa na teknolojia ya sensor-shift stabilization (IBIS).

Mbali na hayo iPhone 13 na iPhone 13 Mini, zote zinakuja na uwezo wa kuchukua video za hadi 4K kwa fps 24, 30, na 60. Pia utaweza kuchukua video za 1080p kwa fps 30, 60, 120 na 240.

Kwa upande wa kamera ya mbele, simu hizi zinakuja na ukingo wa juu au notch ambayo ni ndogo zaidi kuliko iPhone 12, huku ukingo huo ukiwa umehifadhi kamera ya Megapixel 12 ambayo ni (wide), huku ikiwa inasaidiwa na teknolojia za HDR pamoja SL 3D.

Uhifadhi wa Ndani (ROM)

Mabadiliko ya Muhimu Kwenye Simu za iPhone 13 na 13 Mini

Kitu kingine cha tofauti kwenye simu hizi mpya za iPhone 13 na iPhone 13 Mini ni pamoja na uhifadhi wa ndani au ROM, ambapo simu hizi sasa zinapatikana kwa machaguo kati ya GB 128, GB 256 pamoja na GB 512. Simu zote za iPhone 13 na iPhone 13 Mini zinakuja na RAM ya GB 6.

Mengine

Mabadiliko ya Muhimu Kwenye Simu za iPhone 13 na 13 Mini

Mambo mengine ya muhimu kufahamu kuhusu iPhone 13 na iPhone 13 mini ni pamoja na mfumo mpya wa iOS 15 ambao utakuja na simu hizi moja kwa moja.

Usinunue Simu ya Android au iPhone ya Zamani

Kwa upande wa processor simu hizi zinaendeshwa na processor ya Apple A15 Bionic (5 nanometer), ambayo inakuja na CPU ya Hexa-core (2 + 4) pamoja GPU ya Apple yenye 4-core graphics.

Kwa upande wa battery, iPhone 13 na 13 Mini bado hazijulikani zinatumia battery yenye ukubwa kiasi gani, lakini kwa mujibu wa Apple simu hizi zitakuwa na uwezo wa kudumu na chaji zaidi kuliko simu za iPhone 12.

Mbali na hayo, simu zote za iPhone 13 zinakuja na teknolojia ya Fast charging yenye uwezo wa hadi 20W, ambayo kwa mujibu wa Apple ina uwezo wa kuchaji iPhone 13 na 13 Mini kwa hadi asilimia 50 kwa muda wa dakika 30.

Hitimisho

Kwa maoni yangu hayo ndio mambo ya muhimu kwenye simu hizi mpya za iPhone 13 na 13 Mini. Kama unavyoweza kuona mabadiliko hayo ni madogo hivyo kama wewe ni mmiliki wa iPhone 12 pengine huna haja ya kununua iPhone 13 kwa sasa.

Nachokushauri ni ku-update simu yako kwenda kwenye mfumo mpya wa iOS 15 na utaweza kufurahisi zaidi simu yako kuliko kwenda kununua simu mpya yenye sifa zinazo fanana.

Anyway hayo ni maoni yangu sijui wewe unaonaje kuhusu iPhone 13 na 13 Mini, je ni simu ambazo ungependa kununua..? Tuambie kwenye maoni hapo chini.

Kama unataka kujua sifa zaidi na bei ya simu hizi unaweza kusoma hapa, pia endelea kutembelea Tanzania tech kujua zaidi kuhusu iPhone 13 Pro na iPhone 13 Pro Max.

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.