Jinsi ya Kuondoa (Uninstall) Apps Zaidi ya Moja kwa Wakati Mmoja

Pia kupitia njia hii utajua apps zenye kuchukua nafasi kubwa kwenye simu yako
Jinsi ya Kuondoa (Uninstall) Apps Zaidi ya Moja kwa Wakati Mmoja Jinsi ya Kuondoa (Uninstall) Apps Zaidi ya Moja kwa Wakati Mmoja

Ni wazi kuwa mara nyingi kuna wakati unakuta simu imejaa apps nyingi ambazo hata huzitumi kwa wakati huo, lakini pia inapokuja swala la kufuta au (Uninstall) apps hizo bado pia inakuwa ni mthiani sana kwani ni lazima kuondoa app moja baada ya nyingine.

Kuliona hilo leo nimekuletea njia rahisi ambayo unaweza kutumia kuondoa (Unistall) app zaidi ya moja kwa wakati mmoja.

Kumbuka njia hizi ni maalum kwa watumiaji wa simu za Android pekee, kama unatumia simu ya iPhone endelea kutembelea Tanzania Tech tutakuletea njia hii hivi karibuni. Kama unatumia simu ya Android basi moja kwa moja twende pamoja tukajifunze njia hii rahisi ambayo inaweza kusaidia kuongeza nafasi kwenye simu yako kwa haraka na urahisi.

Advertisement

Kwa kuanza unacho takiwa kufanya ni kuingia kwenye soko la Play Store, kisha bofya vitufe vitatu vya Menu vilivyoko juu upande wa kushoto, kisha bofya sehemu ya My apps and games. Baada ya hapo utapelekwa kwenye ukurasa wenye masasisho (update) mapya ya app ulizo pakua, moja kwa moja bofya sehemu iliyo andikwa installed. Baada ya hapo bofya sehemu ya Storage kama inavyo onekana kwenye picha hapo chini.

Jinsi ya Kuondoa (Uninstall) Apps Zaidi ya Moja kwa Wakati Mmoja

Baada ya kubofya hapo ukurasa mpya utafunguka ukiwa na listi ya apps ambazo ume install kwenye simu yako, kupitia hapa utaweza kujua apps ambazo hazijatumika kwa muda mrefu, apps ambazo ni kubwa sana na apps ambazo Google wanakushauti uweze kuziondoa kwenye simu yako.

Melezo yote hayo unaweza kuyapata kwa kubofya kitufe cha kuchuja au (Filter) kilichopo upande wa kulia juu sehemu iliyo andikwa Alphabetical. Bofya hapo kisha chagua menu yoyote kati ya

Jinsi ya Kuondoa (Uninstall) Apps Zaidi ya Moja kwa Wakati Mmoja

  • Recommended – Apps ambazo Google wanakushauri kuondoa (Uninstall) zitakuwa juu.
  • Size – Apps zenye kuchukua nafasi kubwa kwenye simu yako zitakuwa juu.
  • Data usage – App ambazo haijatumiwa kwa muda mrefu zitakuwa juu.
  • Alphabetical – Hapa utaweza kuchagua kupanga apps kwa kufuatana na Alphabet.

Baada ya kuchagua Menu moja kati ya hizo, sasa chagua app unazotaka kuzifuta kwa kuweka tiki mbele ya jina la app husika. Kwa chini utaweza kuona kiasi cha MB au GB unazoweza kuongeza kwenye simu yako baada ya kufuta app hizo, bofya hapo kisha malizia kwa kubofya Free up MB sehemu itakayo tokea kwenye kichumba maalum kama unavyoweza kuona kwenye picha hapo chini.

Jinsi ya Kuondoa (Uninstall) Apps Zaidi ya Moja kwa Wakati Mmoja

Baada ya hapo App hizo zita ondolewa moja kwa moja kutoka kwenye simu yako na utakuwa umeweza kuondoa apps nyingi kwa wakati mmoja kupitia simu yako ya Android.

Kama kutakuwa kuna mahali umekwama usisite kutuandikia kupitia sehemu ya moani hapo chini, kwa maujanja zaidi kama haya hakikisha una tembelea channel yetu ya Tanzania Tech kupitia YouTube kwani huko utaweza kujifunza kwa vitendo.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use