in

YouTube Kuzindua Sehemu Mpya ya Shorts Hivi Karibuni

Utaweza kurekodi video kama vile video za TikTok

YouTube Kuzindua Sehemu Mpya ya Shorts Hivi Karibuni

YouTube imekuwa ikifanya majaribio ya sehemu ya Shorts kwa muda mrefu, sehemu hiyo imeonyesha matokeo makubwa sana ilipokuwa inafanyiwa majaribio kwa nchi za India na sasa nchini Marekani.

Kwa mujibu wa tovuti ya GSMArena, sehemu hii inatarajiwa kuja duniani kote hivi karibu. Sehemu hii inafanana kabisa na jinsi app ya TikTok inavyofanya kazi hivyo tegemea kuona aina zilezile za video ambazo zinafanana na zile zinazo patikana kwenye mtandao wa TikTok.

Kwa sasa sehemu hii bado ipo kwenye majaribio na pengine tunaweza kuona sehemu hii ikija hapa Tanzania na duniani kote kuanzia mwezi huu hadi mwezi wa tano mwaka huu 2021.

Kwa habari zaidi kuhusu sehemu hii na sehemu nyingine kwenye mtandao wa YouTube hakikisha unajiunga nasi hapa, pia endelea kutembelea Tanzania tech kupata habari zaidi.

Jinsi ya Kuanzisha Podcast kwa Urahisi na Bure (100%)

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.