in

Jinsi ya Kutumia Adobe Photoshop 2021 Bure Mwaka Mzima

Utaweza kutumia Adobe Photoshop 2021 kwa mwaka mzima Bure

Jinsi ya Kutumia Adobe Photoshop 2021 Bure Mwaka Mzima

Kama wewe ni mmoja wa watu ambao wanatumia zaidi programu za Adobe hasa adobe photoshop basi ni wazi kuwa unajua kuwa toleo jipya la Adobe Photoshop 2021 limetoka rasmi. Toleo hili ambalo limepewa version namba v22.1.0.94 linakuja na maboresho mengi sana.

Kama unataka kujua zaidi kuhusu maboresho hayo, unaweza kusoma zaidi kupitia ukurasa huu.

Sasa kwa sasa zipo njia nyingi za kupata toleo la bure la programu za Adobe Photoshop, unaweza kusoma makala yetu iliyopita kama unataka kupata toleo zima la programu zote za Adobe kwa mwaka 2019. Lakini kama unataka toleo la Adobe Photoshop 2021 basi unaweza kufuata njia hii.

Kwa kuanza hakikisha unayo Internet kwenye kompyuta yako, hakikisha unayo angalu GB 3 au GB 2 hivi ili kuweza kupakua mfumo mzima wa Adobe Photoshop 2021.

Kama unavyo vyote basi moja kwa moja unachotakiwa kufanya ni kubofya link hapo chini. Kisha moja kwa moja utapelekwa kwenye ukurasa ambao utaweza kupakua toleo jipya la Adobe Photoshop 2021.

Tumia Kamera ya Simu Kama WebCam ya Kompyuta

Pakua Programu Hiyo Hapa

Baada ya kumaliza kudownload tumia programu ya Zip kuweza kufungua file kwa ajili ya ku-install, unaweza kupata programu ya Zip hapa. Pia kumbuka wakati unataka kuextract au ku-unzip file hizo unatakiwa kuweka password na hakikisha unaweka 123 kisha bofya OK.

Jinsi ya Kutumia Adobe Photoshop 2021 Bure Mwaka Mzima

Baada ya hapo Install programu yako na moja kwa moja utaweza kutumia Adobe Photoshop 2021 bure bila kufanya kitu cha ziada. Kifupi ni kuwa tayari programu hii iko Activated na utaweza kutumia bure bila kikwanzo chochote.

Jinsi ya Kutumia Adobe Photoshop 2021 Bure Mwaka Mzima

Kumbuka programu hii ni toleo la Adobe Photoshop pekee, kama unataka matoleo mengine ya Adobe kama vile After Effect na nyingine unaweza kusoma makala yetu iliyopita. Kwa maujanja zaidi endelea kutembelea Tovuti ya Tanzania tech.

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.