in

Gazeti Lite : Soma Habari Mpya Bila Internet (Android)

Soma habari zote kutoka Tanzania bila kutumia Internet kila mara

Gazeti Lite : Soma Habari Mpya Bila Internet (Android)

Najua wengi wenu mnaijua app ya Gazeti, app hii inakupa nafasi ya kusoma hapa mpya bila kuwepo matangazo, lakini pamoja na review nzuri ambazo tumezipata kupitia Play Store tumaona kuna haja ya kuleta app mpya ya Gazeti Lite.

App ya Gazeti Lite inakupa uwezo wa kusoma habari mbalimbali za hapa Tanzania kutoka kwenye vyanzo bora hapa Tanzania. Pamoja na kuwa watu wengi hutumia Opera News lakini wote tunakubaliana kuwa app ya Opera News imekuwa ikileta habari ambazo kuna wakati unakuta ni habari ya miaka hata miwili iliyopita.

Pia wakati mwingine app hii huleta makala nyingi zilizo tafsiriwa ambazo ukweli hazina maadili japo kuwa makala hizo zinapendwa na watu wengi sana hapa Tanzania hasa vijana.

App ya Gazeti Lite inakupa uwezo wa kusoma habari bila Internet na pia utaweza kupata habari mpya kila siku ikiwa pamoja na kusoma magazeti, kusikiliza Radio na vipindi mbalimbali bila kusahau uwezo wa kuanzisha mijadala kupitia Jamii Forums.

Haya hapa baadhi ya mambo unavyoweza kufanya kupitia app ya Gazeti Lite.

  • Utaweza kusoma habari kutoka kwa vyanzo zaidi ya 20 vinavyo aminika
  • Utaweza kisikilza radio kama Clouds FM, Global Radio na vipindi mbalimbali, pia utaweza kudownload vipindi hivyo kwaajili ya kusikiliza baadae.
  • Utaweza kusoma mijadala kupitia tovuti ya jamii forums, pia utaweza kuanzisha na kujibu mijadala hiyo kwa urahisi kupitia app ya Gazeti Lite.
  • Utaweza kusoma habari bila Internet, yani baada ya kufungua app hii subiri iweze kusave habari mpya kisha unaweza kuzima Internet na kuendelea kusoma habari zote zilizopo.
  • Pia utaweza kupata muonekano wa Giza ambao utasaidia kulinda macho yako hasa wakati wa usiku.
  • Pamoja na mambo mengine mengi.

Jaribu app ya Gazeti kisha unaweza kutoa maoni yako unaonaje kupitia ukurasa wake wa Play Store, bado tunaendelea kuboresha app hii hivyo maoni na mawazo mapya yana karibishwa.

Gazeti Lite : Soma Habari Mpya Bila Internet (Android)

Kama umependa ulichosoma na unataka kujaribu app ya Gazeti Lite basi unaweza kudownload app hii kupitia Link hapo chini.

Download Gazeti Lite

Kama una maon, maswali au ushauri unaweza kutuandikia kupitia sehemu ya maoni hapo chini.

Apps Nzuri za Kujaribu Kwenye Simu Yako ya Android (2021)

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.