Ugumu na Ubora wa Simu Yenye Kamera Chini ya Kioo

ZTE Axon 20 5G ni simu ya kwanza yenye kamera ya mbele chini ya kioo
Ugumu na Ubora wa Simu Yenye Kamera Chini ya Kioo Ugumu na Ubora wa Simu Yenye Kamera Chini ya Kioo

Kama wewe ni mfuatiliaji wa Tanzania tech hasa kipengelea cha simu mpya basi ni wazi kuwa unafahamu kuhusu simu mpya ya ZTE Axon 20 5G, simu hii imeshika vichwa vya habari sana siku za karibuni kutokana na kuwa simu ya kwanza kuwa na kamera ya mbele chini ya kioo.

Kifupi ni kwamba, ZTE Axon 20 5G inakuja na kioo kizima yani full display ambapo hakuna kingo kubwa kama simu nyingine, na pia haina hata sehemu ya spika ya kusikilizia simu kwani nayo inapatikana chini ya kioo.

Ugumu na Ubora wa Simu Yenye Kamera Chini ya Kioo

Advertisement

Kama unavyoweza kuona simu hii inakuja na kioo kitupu na pia inakuja na spika iliyopo chini ya kioo pamoja na sehemu ya ulinzi ya fingerprint nayo inapatikana chini ya kioo. Lakini je vipi kuhusu ubora na ugumu wa simu hii mpya. Kufahamu hayo unaweza kuangalia video hapo chini.

Tayari ZTE Axon 20 5G inapatikana kote duniani ikiwa pamoja na Uingereza, Korea Kusini, Urusi, Thailand, Malaysia, Ufilipino, UAE, Saudi Arabia na Afrika Kusini. Kama tayari simu hii inapatikana Afrika kusini basi siku sio nyingi utaweza kununua simu hii hapa nchini Tanzania.

Kumbuka simu hizi zinapatikana kwa matoleo mawili ZTE Axon 20 5G na ZTE Axon 20 4G, unaweza kuangalia tofauti ya simu hizi hapa.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use