in

Serikali ya India Yafungia App ya AliExpress na Nyingine 42

Mbali na App hiyo ya AliExpress, India pia imefungia app nyingine za Alibaba group

Serikali ya India Yafungia App ya AliExpress na Nyingine 42

Kama wewe ni mmoja wa watu ambao wanategemea kusafiri kwenda nchini India basi ni muhimu kujua kuwa apps mbalimbali ambazo zinamilikiwa na kampuni za kichina ikiwemo TikTok na nyingine kama AliExpress zote zitakuwa hazifanyikazi.

Kwa mujibu wa serikali ya India, Sababu za kufungiwa kwa application hizo ni sawa na sababu zile ambazo zilitolewa wakati app ya Tik Tok ilipo fungiwa mapema miezi kadhaa iliyopita, ambapo india iliainisha kuwa pamoja na sababu nyingine apps hizo sio salama kwa matumizi kwa wananchi wake.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Kwa sasa serikali ya India imefungia zaidi ya apps 210 ambapo hii ni pamoja na app zilizotangazwa kwenye taarifa ya mwezi wa 9 na mwezi wa 6 mwaka 2020.

Serikali ya India Yafungia App ya AliExpress na Nyingine 42

Mbali na app ya AliExpress, app nyingine zilizo fungiwa ambazo zinajulikana ni pamoja na app za Alibaba group kama vile Alibaba Workbench, AliSuppliers Mobile App, pamoja na Alipay Cashier. List ya apps nyingine zilizo fungiwa ni kama inavyo onekana hapo chini.

Serikali ya India Yafungia App ya AliExpress na Nyingine 42

Serikali ya India Yafungia App ya AliExpress na Nyingine 42

Kwa sasa baadhi ya wamiliki wa app hizo kama vile app ya PUBG tayari zipo kwenye mazungumzo na serikali ya India kuweza kurudisha app hiyo kwa watumiaji wa nchini India.

Serikali ya India Yafungia App ya AliExpress na Nyingine 42
Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Elon Musk Azindua Mfumo wa Akili Bandia (AI) xAI Grok

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.