in

Kampuni ya Infinix Kumalizia Mwaka na Simu Mpya ya Note

Hatimaye jiandae na simu mpya ya Infinix Note mwaka huu

Kampuni ya Infinix Kumalizia Mwaka na Simu Mpya ya Note

Infinix mbioni kutamba tena na toleo la NOTE na hii ni baada ya toleo la awali la Infinix NOTE 7 vizuri sokoni. kupitia mtandao wao @infinixmobiletz wameashiria kuna ujio wa simu mpya yenye sifa zifuatazo;

• Helio G80 processor
• 64MP Ultra HD 6 kamera
• 5200mAh battery.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Huku ikiwa kampuni haijataja ni toleo gani hilo lakini wadau wa simu za Infinix wamekuwa wakitabiri huwenda toleo hilo jipya ni Infinix NOTE 8 na kutokana na baadhi ya sifa nilizotaja hapo juu. Inasemekana toleo la NOTE ni moja ya toleo lenye ubora kama ilivyo kwa toleo la Infinix ZERO.

Tukiwa bado hatujafahamu sifa nyengine za simu hiyo inayosemekana huenda ni Infinix NOTE 8 lakini tunafahamu Infinix ni kampuni imara yenye kuzalisha simu zenye viwango vya hali ya juu kwa bei ambayo Mtanzania mwenye uchumi wa hali yoyote anaweza kuimudu.

Kwa uchache wa sifa tulizozinyaka inaonekana simu hiyo itakuwa tishia kutokana na aina ya processor Helio G80 kuwa processor yenye kuhimili application zenye ujazo wowote.

Kampuni ya Infinix Kumalizia Mwaka na Simu Mpya ya Note Kampuni ya Infinix Kumalizia Mwaka na Simu Mpya ya Note

Processor ya Helio G80 pamoja ya kuhimili application zenye ujazo mkubwa lakini pia inapunguza kasi ya simu kuisha chaji, inazuia simu isipate moto kwa matumizi ya muda mrefu na kuziendesha application kama za games na nyenginezo pasipo kuzembea zembea.

Kampuni ya Infinix Kumalizia Mwaka na Simu Mpya ya Note

Bado maswali yanabaki kwetu hadi pale tutakapompata Aisha Karupa Afisa wa mahusiano wa kampuni ya Infinix azungumze nasi simu hiyo ni simu gani, sifa nyengine za simu hiyo na bei yake.

Kampuni ya Infinix Kumalizia Mwaka na Simu Mpya ya Note
Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Infinix na JBL Waungana Tena Na Sasa Ni Infinix Note 40

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

One Comment

  1. nimekuwa mfuatiliaji wa maujanja yenu hapa mtandaoni, tatizo Kila niki-click kwenye link YOYOTE Ina cancel kwa kusema Tanzania Tech has stopped. nifanyaje? niliwahi ku-unstall app na ku-install upya bado tatizo halijaisha