in

Infinix Yazindua Rasmi Toleo Jipya la Simu ya Infinix HOT 10

Ni simu iliyotokea kupendwa na vijana zaidi kwa simu zenye thamani ya TZS 350,000

Infinix Yazindua Rasmi Toleo Jipya la Simu ya Infinix HOT 10

Kampuni bingwa ya uzalishaji wa simu za mkononi ya Infinix Mobile imetangaza rasmi uwepo wa toleo jipya katika matoleo ya HOT. Infinix HOT 10 iliingia rasmi mwanzoni mwa week hii katika maduka ya simu nchini Tanzania na kufanya vizuri zaidi ya simu zote zenye thamani ya Sh.300,000 had Sh.350,000. Ni simu iliyotokea kupendwa na vijana zaidi na hii ni kwa sababu imebeba sifa zifuatazo kama vile

Processor aina ya MediaTek Helio G70, battery yenye ujazo wa 5200mAh, kamera zenye megapixel 16+2+2+QVGA kwa megapixel 8 selfie, memory yenye GB 64 + GB 3 RAM, kioo cha nchi 6.78 na teknolojia ya DTS Audio.

Infinix Yazindua Rasmi Toleo Jipya la Simu ya Infinix HOT 10

Infinix HOT 10 ni simu yenye kuwalenga vijana wa kisasa wenye kupenda kwenda na wakati lakini pia ni simu ya kwanza katika matoleo ya HOT Series kuwa na processor yenye kasi aina ya MediaTek Helio G70 na teknolojia ya MediaTek HyperEngine. MediaTek HyperEngine inakazi nyingi katika uchezaji games na kazi moja wapo ni kubeba na kuendesha games zenye ujazo mkubwa pasipo kuzidiwa mzigo.

Kampuni ya Airtel ya Kwanza Kuja na eSIM Tanzania

Kioo cha Infinix HOT 10 chenye Inch 6.78 kumsaidia mtumiaji kuweka application zake katika mpangilio mzuri na kuziona katika hali ya ukubwa zaidi. Infinix HOT 10 haina mvuto katika upande wa kioo tu lakini hata umbo lake linawembamba wa mm9, hivyo unaweza kuihifadhi hata katika mfuko wa suruali au shirt pasipo kuharibu show ya muonekano wako.

Teknolojia ya AI yenye megapixel 8 za selfie na megapixel 16 zinapiga picha zenye uhalisia pasipo kujali nyakati wala mazingira, kamera hizi mbili zina teknolojia ya AI smart beautification na super night view mode kwajili ya ung’arishaji picha katika nyakati zote.

“Battery ya HOT 10 yenye ujazo wa mAh 5200 inadumu na chaji kwa kipindi cha muda mrefu hata pasipo kuzima data ya simu yako na huku ukiendelea kucheza game na kujibu rudisha na mziko mzuri unaochunjwa kwa kutumia teknolojia ya DTS Audio” alisema Afisa wa Mahusiano wa Kampuni ya simu Infinix Mobility, Aisha Karupa.

Usinunue Simu ya Android au iPhone ya Zamani

Infinix HOT 10 inapatikana katika rangi mbalimbali kwenye maduka yote ya simu nchini Tanzania na ili kufahamu zaidi kuhusiana na bidhaa za Infinix tafadhali tembelea @infinixmobiletz .

Written by Jackline John

Jack ni mpenzi wa teknolojia napenda kuandika kuhusu maujanja, simu na kompyuta. Unaweza kunipa maujanja kupitia [email protected]

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.