Hatimaye Simu Mpya ya Infinix ZERO 8 Yafika Rasmi Tanzania

Simu hii inapatikana hapa Tanzania kwa bei kuanzia TZS 750,000
Hatimaye Simu Mpya ya Infinix ZERO 8 Yafika Rasmi Tanzania Hatimaye Simu Mpya ya Infinix ZERO 8 Yafika Rasmi Tanzania

Mara baada ya tetesi za muda mrefu juu ya ujio wa Infinix ZERO 8, hatimaye kampuni ya simu ya Infinix kupitia mitandao yake ya kijamii @infinixmobiletz wameitambulisha rasmi Infinix ZERO 8.

Kwa mujibu wa kampuni ya Infinix, Infinix ZERO ndio kinara ‘flagship model’ kwa mwaka huu wa 2020 na ikiwa kama simu yenye kuiwakilisha kampuni ya Infinix, Infinix ZERO 8 imebeba sifa lukuki kama zifuatazo;

Advertisement

Simu hii inakuja na MTK Helio G90T processor, RAM ya GB 8 ROM ya GB 128, vyote vikiwa vinaifaya Infinix ZERO 8 kuwa na ufanisi zaidi wa kufungua kubeba files, videos na games zenye ukubwa wa aina yoyote pasipo kugoma goma. Vile vile Infinix ZERO 8 ina teknolojia ya 3D ambayo hii ni maalumu kwa ajili ya kupunguza joto la simu endapo utaitumia simu yako kwa muda mrefu.

Hatimaye Simu Mpya ya Infinix ZERO 8 Yafika Rasmi Tanzania

Infinix ZERO 8 ina kamera zenye kubeba megapixel kubwa, nyuma ikiwa ni Megapixel 64 selfie ikiwani Megapixel 48, kamera hizo zimetengenezwa kwa sensor ya IMX686 Sensor ambayo ni maalumu kwa ajili ya kupiga picha kali na zenye uhalisia pasipo kujali muda wala mazingira.

Hatimaye Simu Mpya ya Infinix ZERO 8 Yafika Rasmi Tanzania

Infinix ZERO 8 inauwezo wa kudumu na chaji kwa zaidi ya siku moja kutokana na matumizi yako, huku uwezo wake mkubwa wa battery ya 4500 mAh ukikuwezesha kutumia simu hiyo bila wasiwasi, mbali na hayo simu hii inakuja na teknolojia ya Fast Charging 33W Super yenye uwezo wa kufanya simu hii kujaa chaji kwa haraka ndani ya muda mfupi.

Muonekano wa Infinix ZERO 8 ni premium, na ukweli naweza kusema simu hii inakuja na desgin ya kuvutia sana kutokana na muundo wake kuwa mwembamba na wigo mpana wa kioo cha inch 6.85 FHD+.

Hatimaye Simu Mpya ya Infinix ZERO 8 Yafika Rasmi Tanzania

Kwa sasa Infinix ZERO 8 ipo Tanzania na unaweza kuipata katika maduka yote ya simu kwa bei isiyozidi Tsh.750,000/=

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use