in

Picha Halisi za Simu Mpya ya Samsung Galaxy Note 20

Hizi hapa picha halisi za Samsung Galaxy Note 20

Picha Halisi za Simu Mpya ya Samsung Galaxy Note 20

Wakati ikiwa zimebaki siku chache hadi kampuni ya Samsung kuzindua simu mpya ya Galaxy Note 20, hivi karibuni zimevuja picha ambazo zinazo onyesha muonekano halisi wa simu hiyo.

Kwa mujibu wa tovuti ya GSMArena, picha hizo zime vujishwa kwa bahati mbaya na Samsung wenyewe huku ikiwa ni katika harakati za kuandaa uzinduzi wa simu hizo mpya.

Picha Halisi za Simu Mpya ya Samsung Galaxy Note 20

Kama ilivyo semekana kwenye tetesi, simu mpya za Galaxy Note 20 zitakuja na mfumo mpya wa kamera tatu, huku kamera kuu ikiwa na Megapixel 108, na kamera nyingine mbili zikiwa na megapixel 13 na Megapixel 12.

Kamera hizo kwa pamoja zinasemekana kuwa na uwezo wa kuchukua video za hadi 8K, huku zikiwa na teknolojia nyingine kama Super Steady video, HDR10+ na nyingine nyingi.

Hata hivyo inasemekana simu hii kwa mbele itakuja na kamera kubwa ya Megapixel 40, huku ikiwa na uwezo wa kuchukua video za hadi 4K. Kamera hiyo pia inasemekana kusaidiwa na teknolojia za Dual video call, na Auto-HDR.

Fahamu eSIM Mfumo Mpya wa Laini za Simu za Kidigitali

Picha Halisi za Simu Mpya ya Samsung Galaxy Note 20

Kwa sasa Note 20 inategemea kuzinduliwa kwa matoleo mawili, toleo la kwanza likiwa ni toleo la kawaida na toleo la pili likiwa ni Note 20 Pro. Kwa sasa bado hakuna taarifa zaidi, ila simu hizi zinategemewa kuzinduliwa mwezi ujao.

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.