in

Video : Ugumu na Ubora wa Samsung Galaxy Z Flip

Je simu hii inafaa kwa soko la Afrika.?

Video : Ugumu na Ubora wa Samsung Galaxy Z Flip

Baada ya kampuni ya Samsung Kuzindua simu mpya ya Galaxy Z Flip, hatimaye leo karibu uweze kujionea ugumu na ubora wa simu hii mpya ya kujikunja kutoka Samsung. Kabla ya kuangalia video hii pengine mimi nikupe maoni yangu binafsi.

Kwangu mimi naona kama simu hizi za kujikunja hasa kwa hapa Tanzania bado hazina nafasi sana na nisingependa kutoa ushauri wa moja kwa moja kwa mtu kununua simu hizi, hii ni kutokana na ubora wa simu hizi kuwa mdogo ukilinganisha na kiasi cha pesa mtumiaji anacho lipia.

Ni vyema kuendelea kusubiri hadi hapo simu hizi zitakapo kuwa nyingi kwani natumaini kwa muda huo simu hizo zitakuwa na ubora zaidi kwani kampuni hizo zitakuwa zimegundua madhaifu mengi kwenye simu hizo na kurekebisha madhaifu hayo kutokana na maoni kutoka kwa watumiaji. Basi kwa kusema hayo sasa endelea na angalia ugumu na ubora wa simu hii.

 

Angalia Hapa Mubashara Uzinduzi wa iPhone 14

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.