in

Jiandae na Galaxy A01 Simu ya Bei Rahisi Kuliko Galaxy A10

Simu nyingine ya bei rahisi kutoka Samsung inakuja hivi karibuni

Jiandae na Galaxy A01 Simu ya Bei Rahisi Kuliko Galaxy A10

Kama ulikuwa unadhani Samsung Galaxy A10 ndio simu ya bei rahisi pekee kutoka Samsung basi jiandae na simu mpya ya Galaxy A01. Kwa mujibu wa tovuti ya Geekbench ambayo hutumika kuonyesha majaribio ya simu mbalimbali kabla ya kutoka, Galaxy A01 inategemewa kutoka hivi karibuni huku ikiwa na sifa za kawaida.

Kwa mujibu wa tovuti hiyo, Galaxy A01 inategemea kuja na RAM ya GB 2 pamoja na processor ya Octa core pamoja na battery ya kubwa ya 3,000mAh. Mbali na sifa hizo, kupitia tovuti hiyo ya Geekbench pia kuna muonekano wa ndani wa simu hiyo pamoja na ramani ya simu hii jinsi itakavyokuwa.

Jiandae na Galaxy A01 Simu ya Bei Rahisi Kuliko Galaxy A10

Jiandae na Galaxy A01 Simu ya Bei Rahisi Kuliko Galaxy A10

Kama unavyoweza kuona kwenye picha hapo juu, Galaxy A01 inategemea kuja na kamera mbili kwa nyuma, pia kama unavyoweza kuona sehemu ya headphone jack itakuwepo. Pia kwa mujibu wa tetesi simu hii inasemekana kuja na uhifadhi wa ndani wa GB 16 pamoja na kioo chenye ukubwa wa inch 5.7.

Angalia Hapa Mubashara Uzinduzi wa iPhone 14

Jiandae na simu mpya ya Samsung Galaxy A51

Kujua sifa kamili za simu hii pamoja na siku itakapo zinduliwa rasmi hakikisha unaendelea kutembelea tovuti ya Tanzania Tech kila siku, pia kama unataka kujua sifa na bei ya smartphone, laptop na vitu vingine mbalimbali basi tembelea tovuti yetu mpya ya Price in Tanzania Hapa.

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

One Comment