in

Kutana na App Inayokupa Uwezo wa Kujaribu Viatu Kabla ya Kununua

Kupitia app hii utaweza kujaribu kiatu kabla ya kununua

Kutana na App Inayokupa Uwezo wa Kujaribu Viatu Kabla ya Kununua

Katika ulimwengu huu wa sayansi na teknolojia ni wazi kuwa huna haja tena ya kununua kitu usicho kipenda kutokana na kuwa na vyanzo vingi sana vya kupata taarifa za bidhaa unayotaka kununua hata kabla ya kununua.

Lakini wote tunakubaliana kuwa hii ni rahisi sana kama unataka kununua kifaa cha kieletroniki kama vile simu, kompyuta au kifaa chochote kinacho tuzxmia umeme. Lakini je, kwa upande wa nguo au viatu ulishawahi kujiuliza unafanyaje..? Je unawezaje kujua sifa za viatu au nguo..?

Sasa karibu kwenye ulimwengu mpya wa teknolojia, kupitia simu yako sasa unaweza kujaribu viatu hata kabla ya kwenda kununua viatu hivyo. Kupitia app inayoitwa Wanna Kicks, sasa utaweza kutumia simu yako kuweza kujaribu viatu mbalimbali moja kwa moja kabla ya kununua..”nimesikia umeuliza kivipi“..?

Kama unavyoweza kuona hapo juu kwenye video, unachotakiwa kufanya ni kupakua app ya Wanna Kicks kwenye simu yako ya Android au iOS kisha washa app hiyo na elekezea kamera ya kwenye miguu yako puffff…  moja kwa moja utaweza kuna kiatu kwenye mguu wako kupitia kamera ya simu yako.

Apps Nzuri za Android Kwaajili ya Kulinda Afya Yako

Uzuri ni kwamba unaweza kuangalia pande zote za kiatu kwa kugeuza mguu wako kushoto kulia pia kwa juu na hata kwa nyuma, mbali na hayo unaweza kuchukua picha ukiwa umevaa viatu hivyo na moja kwa moja utaweza kushare na ndugu na jamaa au hata muuza duka la viatu unapotaka kununua viatu vya namna hiyo.

Kutana na App Inayokupa Uwezo wa Kujaribu Viatu Kabla ya Kununua

Ndani ya App kuna viatu vya brand mbalimbali kama vile Nike, Adidas, Puma na viatu vungine vingi, unachotakiwa kufanya ni kuchagua aina ya kiatu kwa kusogeza sehemu ya chini ya App hiyo. Kama unatala kujaribu app hiyo unaweza kufanya hivyo kwa kupakua app hiyo kupitia hapo chini.

Kama utakuwa umeshinda kutumia app hiyo kwa namna yoyote unaweza kutuandikia kupitia sehemu ya maoni hapo chini, Kwa habari zaidi unaweza kuendelea kusoma hapa kujua app nyingine nzuri ambazo unaweza kutumia kuedit video kupitia simu yako ya Android.

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.