in

Je Wajua Nchi Maarufu Kwa Kutuma Ujumbe Mfupi wa Maneno (SMS)

Nchini humo SMS zaidi ya Bilioni 6.36 zimetumwa kati ya kipindi cha mwaka 2008 hadi 2009

Je Wajua Nchi Maarufu Kwa Kutuma Ujumbe Mfupi wa Maneno (SMS)

Karibu kwenye makala nyingine ya Je wajua, leo tutaenda kuangazia kitu cha tofauti kidogo na tuta angalia zaidi maswala mazima ya ujumbe mfupi wa maneno au SMS.

Kwa kifupi kabisa historia ya SMS sio ya muda mrefu sana kwani SMS ya kwanza kabisa ilitumwa mwaka 1992 na Neil Papworth ambaye alituma SMS hiyo kupitia mtandao wa Vodafone, lakini cha kushangaza Neil hakutuma SMS hiyo kwa kutumia simu kama ilivyo zoeleka bali alitumia kompyuta… anyway kwa kuwa nilisema kwa ufupi unaweza kusoma historia nzima ya SMS Hapa.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Sasa tukirudi kwenye makala hii ya leo, ni wazi mpaka sasa wapo watu wengi ambao bado wanategemea SMS kuliko hata kupiga au hata mitandao kama WhatsApp na Facebook kuweza kuwasiliana, moja ya watu hao ni wananchi wa nchini Philippines.

Kwa mujibu wa tovuti ya Reuters, inasemekana Philippines ndio nchi inayotajwa kwa wananchi wake kutuma SMS nyingi zaidi kuliko nchi nyingine yoyote duniani. Kwa mujibu wa mtandao wa simu wa Philippine Long Distance Telephone Co inasemekana kati ya kipindi cha mwaka 2007 hadi 2008 wananchi wa nchini humo walikuwa wakituma SMS zaidi ya Milioni 700 hadi 750 kwa siku.

Mbali na hayo inasemekana kati ya kipindi cha mwaka 2008/2009 SMS zaidi ya bilioni 6.37 zilitumwa hasa kwenye kipindi cha Christmas na Mwaka Mpya. Hadi sasa inasemekana wafilipino wengi wamegoma kabisa kutumia njia nyingine za mawasiliano kama WhatsApp na kuendelea kutumia SMS zaidi.

Nchi nyingine ambazo zinasemekana kutuma SMS zaidi ni pamoja na Indonesia ( SMS zaidi ya Bilioni 1.193 zinatumwa), Malaysia (SMS zaidi ya Bilioni 1.075 zinatumwa) na Pakistan (SMS zaidi ya Bilioni 763 zinatumwa) hii yote ikiwa ni kati ya kipindi hicho cha mwaka 2008 na 2009.

Kuonyesha kabisa kwamba nchi hizi hadi sasa zinashikilia mataji ya kutuma SMS zaidi, ni nchi moja tu ya Indonesia ambayo ndio iliyotajwa kwenye nchi zinazoongoza kwa kutumia programu ya WhatsApp mwaka 2018. Nchi nyingine bado zinaendeleza utamaduni wao wa kutumia SMS.

Vipi kwa upande wako, je unatumia SMS zaidi kuliko unavyotumia programu za kuchati kama WhatsApp..? Tuambie kwenye sehemu ya maoni hapo chini, hadi siku nyingine kwenye makala ya je wajua endelea kutembelea Tanzania Tech.

Je Wajua Nchi Maarufu Kwa Kutuma Ujumbe Mfupi wa Maneno (SMS)
Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Kutana na Gari Kubwa Kuliko Yote Duniani (Linatembea)

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

One Comment