in

Kampuni ya Apple Yazindua iPad Air (2019) na iPad Mini (2019)

Sifa na bei ya iPad Air (2019) na iPad Mini (2019)

Kampuni ya Apple Yazindua iPad Air (2019) na iPad Mini (2019)

Muda mchache uliopita, kampuni ya Apple imeongeza idadi ya matoleo ya iPad zake kwa kuzindua iPad Air (2019) na iPad Mini (2019). iPad Air (2019) inakuja na kioo cha inch 10.5 na iPad Mini (2019) inakuja na kioo cha inch 7.9.

iPad hizo hazina tofauti kubwa sana zaidi ya ukubwa wa kioo, pamoja na muundo wa iPad hizo. Kwa upande wa iPad Air (2019) yenyewe inakuja na kioo chenye resolution ya 2224×1668 pixel, huku ikiwa na uwiano wa 4:3.

Kampuni ya Apple Yazindua iPad Air (2019) na iPad Mini (2019)

iPad Mini (2019) yenyewe inakuja na kioo chenye resolution ya 2048×1536 pixel pamoja na uwiano wa 4:3. Mbali na hayo sifa nyingine za iPad hizi mpya zinafanana sana kama inavyo onekana kwenye sifa kamili hapo chini.

Kampuni ya Apple Yazindua iPad Air (2019) na iPad Mini (2019)

Sifa za iPad Air (2019)

 • Ukubwa wa Kioo – Inch 10.5 chenye teknolojia ya IPS LCD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1668 x 2224 pixels.
 • Mfumo wa Uendeshaji – iOS 12.1.3.
 • Uwezo wa Processor – Hexa-core (2×2.5 GHz Vortex + 4×1.6 GHz Tempest).
 • Aina ya Processor (Chipset) – Apple A12 Bionic (7 nm) Chipset.
 • Uwezo wa GPU – Apple GPU (7-core graphics).
 • Ukubwa wa Ndani – Ziko iPad za aina tatu simu moja inakuja na GB 64, nyingine GB 256 zote zikiwa hazina uwezo wa Memory Card.
 • Ukubwa wa RAM – GB 2
 • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 7 yenye f/2.2, 31mm (standard), HDR na uwezo wa kuchukua video za [email protected]
 • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Megapixel 8 yenye ff/2.2, 31mm (standard), huku ikiwa inasadiwa na HDR na uwezo wa kuchukua video za [email protected]
 • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Po battery (30.2 Wh).
 • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0 na GPS ya A-GPS, GLONASS, BDS. USB ya 2.0, proprietary reversible connector.
 • Rangi – Inakuja kwa rangi mbili za Silver na Space Gray
 • Mengineyo – Haina Radio FM, Inatumia Line Moja za Nano-SIM / Electronic SIM card (Apple e-SIM), haina sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
 • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, gyro, compass, barometer.
 • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
 • Ulinzi – Inayo Ulinzi Fingerprint (Kwa Mbele)
Usinunue Simu ya Android au iPhone ya Zamani

Bei ya iPad Air (2019)

Kwa upande wa bei ya iPad Air (2019), Tablet hii inasemekana kuanza kuuzwa kwa dollar za marekani $499 ambayo ni sawa na Shilingi za Tanzania Tsh 1,171,000 bila kodi. Kumbuka bei inaweza kuongezeka kutokana na kodi.

Sifa za iPad Mini (2019)

 • Ukubwa wa Kioo – Inch 7.9 chenye teknolojia ya IPS LCD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1536 x 2048 pixels.
 • Mfumo wa Uendeshaji – iOS 12.1.3.
 • Uwezo wa Processor – Hexa-core (2×2.5 GHz Vortex + 4×1.6 GHz Tempest).
 • Aina ya Processor (Chipset) – Apple A12 Bionic (7 nm) Chipset.
 • Uwezo wa GPU – Apple GPU (7-core graphics).
 • Ukubwa wa Ndani – Ziko iPad za aina tatu simu moja inakuja na GB 64, nyingine GB 256 zote zikiwa hazina uwezo wa Memory Card.
 • Ukubwa wa RAM – GB 2
 • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 7 yenye f/2.2, 31mm (standard), HDR na uwezo wa kuchukua video za [email protected]
 • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Megapixel 8 yenye ff/2.2, 31mm (standard), huku ikiwa inasadiwa na HDR na uwezo wa kuchukua video za [email protected]
 • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Ion 5124 mAh battery.
 • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0 na GPS ya A-GPS, GLONASS, BDS. USB ya 2.0, proprietary reversible connector.
 • Rangi – Inakuja kwa rangi mbili za Silver na Space Gray
 • Mengineyo – Haina Radio FM, Inatumia Line Moja za Nano-SIM / Electronic SIM card (Apple e-SIM), haina sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
 • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, gyro, compass, barometer.
 • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
 • Ulinzi – Inayo Ulinzi Fingerprint (Kwa Mbele)
Kampuni ya Nokia Kubadilisha Logo Yake ya "NOKIA"

Bei ya iPad Mini (2019)

Kwa upande wa bei ya iPad Mini (2019), yenyewe inasemekana kuanzia dollar za marekani $399 ambayo ni sawa na Tsh 939,000 bila kodi. Kumbuka bei inaweza kuongezeka kutokana na kodi.

iPad zote zinasemekana kuwa zitapatikana kwa nchi za Australia, Austria, Belgium, Canada, Czech Republic, Denmark, Finland, France, Germany, Hong Kong, Hungary, Ireland, Italy, Japan, Luxembourg, Netherlands, New Zealand, Norway, Poland, Portugal, Singapore, Spain, Sweden, Switzerland, the UAE, UK na US. Kuanzia wiki ijayo iPad hizo zinasemekana kupatikana, nchini China (Wi-Fi ), Macau (Wi-Fi ) na Mexico. Sehemu nyingine ni Colombia, Greece, India, Israel, Russia, Saudi Arabia, South Africa, Thailand (Wi-Fi) na Turkey.

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.