in

Huawei Yazindua Huawei Y5 Lite Yenye Android Go

Zifahamu hizi hapa sifa na bei ya Huawei Y5 Lite

Sifa na bei ya Huawei Y5 Lite

Kampuni ya Huawei bado inaendelea na mapambano ya kukuza mauzo ya simu zake, Baada ya kuzindua simu mpya ya Huawei Y7 Pro (2019), hivi leo kampuni hiyo imezindua tena simu nyingine mpya ya Huawei Y5 Lite.

Kama jina la simu hii linavyosema, Huawei Y5 Lite ni toleo la bei rahisi la simu za Huawei Y5 Prime (2018). Simu hii mpya inakuja ikiwa inendeshwa na mfumo wa Android Go 8.1 (Oreo), mfumo ambao unatumika mara nyingi kwenye simu za Android za bei nafuu. Vilevile Kama unavyo jua kuwepo kwa mfumo wa Android Go inamaanisha simu hii ya Huawei Y5 Lite inakuja na uwezo wa RAM usio pungua GB 1.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Huawei Y5 Lite

Sifa nyingine za simu hii ni pamoja na kioo cha inch 5.45 kilicho tengenezwa kwa teknolojia ya IPS LCD chenye resolution ya 1440×720 pixel, kamera ya nyuma inakuja na uwezo wa Megapixel 8 ikiwa na f/2.0 PDAF, huku kamera ya mbele ikiwa na Megapixel 5 ikiwa na f/2.2 fixed-focus.

Simu hii inatumia processor ya MediaTek MT6739 processor ambayo inasaidiwa na RAM ya GB 1 pamoja na ukubwa wa ndani wa hadi GB 16 unaoweza kuongezewa na memory card hadi ya GB 256. Sifa nyingine za Huawei Y5 Lite ni kama zifuatazo.

y5 lite

Sifa za Huawei Y5 Lite

  • Ukubwa wa Kioo  – Inch 4.45 chenye teknolojia ya IPS LCD, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resoluti ya 720 x 1440 pixels (~295 ppi density)
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android Go 8.1 (Oreo)
  • Uwezo wa Processor – Quad-core 1.5 GHz Cortex-A53.
  • Aina ya Processor – Mediatek MT6739 (28 nm).
  • Uwezo wa GPU – PowerVR GE8100.
  • Ukubwa wa Ndani – GB 16 yenye uwezo wa kuongezewa na memory card hadi GB 256.
  • Ukubwa wa RAM – GB 1.
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 5 yenye f/2.2 pamoja na flash ya LED flash.
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Megapixel 8 yenye f/2.0, PDAF. Kamera  hiyo inasaidiwa na Flash ya LED Flash.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Non-removable Li-Ion 3020 mAh.
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 4.2, A2DP, LE pamoja na GPS ya A-GPS, GLONASS, microUSB 2.0, USB On-The-Go.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi mbili za Blue na Black.
  • Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Aina za Sensor – Accelerometer, proximity na compass
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G.
  • Ulinzi – Haina Fingerprint.

Bei ya Huawei Y5 Lite

Kwa upande wa bei, Simu hii inatarajiwa kuanza kupatikana hivi karibuni kwa kiasi cha Euro €100 ambayo ni sawa na Shilingi za Tanzania Tsh 262,000 bila kodi. Kumbuka bei inaweza kubadilika kutokana na kupanda na kushuka kwa viwango vya kubadilisha fedha vya siku husika pamoja na kodi.

Huawei Yazindua Huawei Y5 Lite Yenye Android Go
Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Infinix na JBL Waungana Tena Na Sasa Ni Infinix Note 40

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.