Hatimaye Kampuni ya ZTE Yazindua Simu Mpya ya Nubia Z18

Zifahamu hizi hapa ndio sifa kamili za Nubia Z18
Nubia Z18 Pic 1 Nubia Z18 Pic 1
Nubia Z18

Jabokuwa kampuni ya ZTE imekuwa na mwaka wa tabu kwa kunyanganywa leseni ya kuuza simu zake nchini marekani, lakini bado kampuni hiyo ya nchini China inaendelea kupambana kwa kuzindua simu yake mpya ya Nubia Z18 huko nchini China.

Simu hiyo mpya ya Nubia Z18 inakuja na kioo cha inch 5.99 inch chenye resolution ya 1080 x 2160 pixel, kioo hicho kimetengenezwa kwa teknolojia ya IPS LCD ambacho pia kinakuja na ukingo mdogo wa juu maarufu kama Top Notch.

Advertisement

Nubia Z18 inakuja na processor ya Snapdragon 845 ambayo inasaidiwa na RAM ya GB 6 au GB 8 pamoja na ukubwa wa ndani wa kuchagua kati ya GB 64 na GB 128. Simu hii pia inakuja na battery yenye ukubwa wa 3,450mAh yenye teknolojia ya Qualcomm’s Quick Charge 4.0. Sifa nyingine za Nubia Z18 ni kama zifuatazo.

Sifa za Nubia Z18

  • Ukubwa wa Kioo  – Inch 5.99 chenye teknolojia ya LTPS IPS LCD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1080 x 2160 pixels, na uwiano wa 18:9 ratio (~403 ppi density).
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.1 (Oreo)
  • Uwezo wa Processor – Octa-core (4×2.65 GHz Kryo 385 Gold au 4×1.8 GHz Kryo 385 Silver).
  • Aina ya Processor (Chipset) – Qualcomm SDM845 Snapdragon 845 Chipset.
  • Uwezo wa GPU – Adreno 630
  • Ukubwa wa Ndani – Ziko simu za aina mbili moja inayo GB 64 na nyingine inayo GB 128 lakini haina uwezo wa kuongezewa na memory card.
  • Ukubwa wa RAM – Ziko simu mbili moja ikiwa na RAM ya GB 6 na nyingine ikiwa na GB 8
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 8 yenye HDR na yenye kuchukua video za 1080p@30fps.
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera mbili kwa nyuma moja ikiwa na Megapixel 24 yenye f/1.6, OIS, dual pixel PDAF na nyingine ikiwa na Megapixel 16 yenye f/1.6, AF. Huku zote zikiwa zinasadiwa na Flash ya Dual-LED dual-tone flash.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Po 3450 mAh battery yenye teknolojia ya Fast battery charging (Quick Charge 4.0) 9V/2A 18W.
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0, A2DP, HD, LE pamoja na GPS ya A-GPS, GLONASS. USB ya Type-C 1.0 reversible connector, USB On-The-Go.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi tatu za Black, Red na Stary Night
  • Mengineyo – Haina Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by),  Haina sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint , accelerometer, gyro, proximity, compass.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa Nyuma).

Bei ya Nubia Z18

Kwa upande wa bei, simu hii inakadiriwa kuuzwa kwa Yuan ya China CNY 2,799 kwa simu yenye RAM ya GB 6 na ukubwa wa ndani wa GB 64 ambayo ni sawa na Tsh 938,000 bila kodi. Kwa toleo lingine la Nubia Z18 lenye ukubwa wa ndani wa GB 128 na RAM ya GB 8 litauzwa kwa Yuan CNY 3,299 ambayo ni sawa na Tsh 1,105,000 bila kodi. Vilevile simu hii inakuja na toleo maalum la van Gogh ambalo litauzwa kwa bei zaidi ya Yuan CNY 3,599 ambayo ni sawa na Tsh 1,206,000 bila kodi. Kumbuka bei inaweza kubadilika kwa hapa Tanzania kutokana na kodi na viwango vya kubadilisha fedha.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use