in

Samsung Kuzindua Simu Inayo Jikunja Mwaka Huu (2019)

Simu ya kwanza ya Samsung inayo jikunja inakuja rasmi mwaka huu 2019

simu inayo jikunja

Kampuni ya Samsung imekuwa ikifanya majaribio mbalimbali ya simu inayo jikunja au (foldable smartphone) tokea mwaka 2012. Hivi karibuni mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo DJ Koh, ambaye alikuwa akihojiwa na kituo cha utangazaji cha CNBC, alisema kuwa simu ya kwanza ya mtindo huo inaweza kuzinduliwa rasmi kupitia mkutano wa wabunifu unaojulikana kama Samsung developer conference ambao hufanyika kila mwaka mwezi November.

Mkurugenzi huyo wa Samsung amedai kuwa simu hizo hzikutoka mapema kwa sababu kwa kipindi hicho chote utengenezaji wa simu hizo umekuwa mkugumu sana lakini hadi sasa matumaini ni makubwa na pengine mwaka huu simu hizo zinaweza kuja rasmi kwa watumiaji.

Mwaka 2012 kampuni ya Samsung ilizindua simu inayojikunja ya kwanza ya majaribio, ambayo haikufanikiwa kuwafikia watumiaji wa simu za Samsung. Hata hivyo kupitia mahojiano hayo na kituo cha CNBC, DJ Koh akubainisha chochote kuhusu simu hizo zaidi ya kusema simu hizo zitawaacha watumiaji wa simu za samsung wakishangaa kwa kusema “wow, this is the reason Samsung made it.

Fahamu eSIM Mfumo Mpya wa Laini za Simu za Kidigitali

Samsung ilizindua Tangazo hilo mwaka 2014 ikiwa na lengo la kutengeneza simu inayo jikunja, kutoka mwaka huo hadi mwaka huu 2019 hatimaye lengo la Samsung litaenda kutimia.

Nini maoni yako kuhusu Samsung kuja na simu za mtindo huu, unadhani simu hizi zinaweza kuondoa simu za kawaida ambazo sasa zinatumika..? Tuambie kwenye sehemu ya maoni hapo chini.

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.