in

Muonekano wa iPhone Xs Wavuja Kabla ya Uzinduzi

Muonekano wa simu mpya ya iPhone Xs wavuja kabla ya kuzinduliwa

Muonekano wa iphone Xs

Kampuni ya Apple ni moja kati ya kampuni zenye msimamo mkali sana kuhusu uvujishaji wa bidhaa zake kabla ya kuzinduliwa rasmi, mwaka jana kampuni ya Apple ilimfukuza kazi mhandisi wake baada ya mtoto wa mhandisi huyo kuonyesha muonekano wa iPhone X kabla ya simu hiyo kuzinduliwa rasmi.

Lakini pamoja na Apple kuwa na msimamo mkali kuhusu uvujishaji wa aina hiyo bado ni ngumu sana kuweza kuzuia uvujishaji kwa asilimia 100 ukizingatia simu hizi hupitia kwenye mikono ya watengenezaji wengi pamoja na makampuni mbalimbali kabla ya kuingia sokoni.

Sasa ikiwa yamebaki masaa kadhaa hadi kuzinduliwa rasmi kwa simu mpya za iPhone Xs, iPhone Xs Plus pamoja na iPhone Xc, tayari kumesha sambaa picha zenye muonekano wa simu mpya inayo tarajiwa ya iPhone Xs. Simu hiyo kwa muundo haitofautiani kabisa na simu ya mwaka jana ya iPhone X ila tu ukubwa wa simu hii ya sasa umeongezwa na kufikia inch 6.8 kutoka ukubwa wa simu ya mwaka jana ya iPhone X ambayo ilikuwa na inch 5.8.

Kwa sasa bado hakuna tetesi yoyote inayoelezea kuhusu sifa za simu hii ila kwa sababu yamebaki masaa machache, basi tukutane kwenye uzinduzi wa simu hizi mpya ambao utonyeshwa mubashara kabisa kupitia hapa Tanzania Tech siku ya leo kuanzia majira ya saa mbili kamili za usiku.

Angalia Hapa Mubashara Uzinduzi wa iPhone 14

Kama wewe ni mpenzi wa bidhaa za Apple nakusihi usikose kutizama uzinduzi huo mubashara kabisa kupitia hapa Tanzania Tech.

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.