Matatizo ya Afya Yanayoletwa na Kutumia Simu Muda Mrefu

Matatizo ya kiafya yanayosababishwa na utumiaji wa Smartphone uliopitiliza
matatizo ya kiafya ya simu matatizo ya kiafya ya simu

Simu ni muhimu sana kwenye maisha yetu ya kila siku, pia kwenye ulimwengu huu wa sasa wa sayansi na teknolojia ni vigumu sana kuishi bila kuwa na simu au kwa lugha ya kingereza (Smartphone).

Lakini pamoja na kuwa simu ni muhimu sana kwenye maisha yetu, ni vyema kukumbuka kuwa chochote kile ambacho utakizidisha sana basi hubadilika na kuwa sumu. Kwa upande wa simu au smartphone nayo pia ni hivyo hivyo kwani yapo matatizo mengi sana ambayo nayo pia yanatokana na utumiaji wa simu au smartphone uliopitiliza.

Sasa kwenye makala hii utaweza kujua matatizo matano ya kiafya ambayo haya hutokea mara nyingi sana na inawezekana kabisa ulikuwa hujui nini chanzo cha matatizo hayo ambayo hutokea mara kwa mara kutokana na utumiaji wa simu kwa muda mrefu.

Advertisement

Kama unamatatizo haya ambayo mengi yanajirudia rudia mara kwa mara ni vyema kumuona daktari au kwenda hospitali au kwenye kituo cha Afya kilichopo karibu na wewe, basi baada ya kusema hayo twende tukangalie matatizo haya.

  • Kuumwa na Kichwa na Kukosa Usingizi

Kuumwa na kichwa ni moja kati ya dalili inayo ashiria mambo mengi sana kwenye mwili wa binadamu, lakini pia kama umekuwa ukiumwa na kichwa mara baada ya kumaliza kutumia simu yako au umekuwa ukikosa usingizi mara kwa mara baada ya kutumia simu yako ya mkononi basi inawezekana tatizo hilo linasababishwa na utumiaji uliopitiliza wa simu yako ya mkononi. Kama unatatizo hili ni vyema kuwa unapumzika kutumia simu yako kwa muda fulani angalau mara 5 au 10 kila siku, pia hakikisha unaachana na tabia ya kutumia simu kabla ya kulala. Kumbuka kama tatizo hili likizidi ni vyema kumuona daktari.

  • Maumivu ya Mgongo au Shingo (Text Neck)

Kutokana na utumiaji wa simu au smartphone uliopitiliza watu wengi huweza kupata ugonjwa wa uti wa mgongo ambao kwa kitaalam unaitwa Text Neck. Ugonjwa huu utokea pale mtu anapotumia simu au smartphone na kujikunja na wakati mwingine mtu hujikunja hadi kufikia uwiano wa nyuzi 60, hii inaweza kuonekana sio ukunjaji wa shingo wa kiasi kikubwa sana lakini kufanya hivyo kwa muda mrefu huweza kusababisha mgandamizo kwenye eneo linalo jikunja na hivyo kufanya mtu kupata maumivu ya mara kwa mara anaponyoosha sehemu hiyo ya shingo. Kuepukana na tatizo hili unashauriwa kutumia simu kwa muda wa kawaida na pia hakikisha unatumia simu kwa usawa sio kwa kujikunja sana. Pia tatizo hilo likizidi usiache kumuona daktari.

  • Kuona kwa Shida au Kuwasha kwa Macho

Kuona kwa shida inaweza ikawa ni chanzo cha magonjwa mengine ya hatari ya macho yako, lakini kama umekuwa ukiona kwa shida mara baada ya kutumia simu yako pengine hiyo ni dalili ya matatizo yanayosababishwa na matumizi ya smartphone yaliyopitiliza. Mara nyingi hii hutokea pale unapotumia simu yako kwa mwanga hafifu sana au kwa mwanga mkali sana. Ni vyema kumuona daktari maalum wa macho pale unapo sikia dalali yoyote ya tofauti kwenye macho yako.

  • Vidole vya Mikono Kufa Ganzi Mara kwa Mara

Kama umekuwa natatizo la kufa ganzi kwenye mikono mara kwa mara ni vyema uwende kumuona daktari, lakini pia kama umekuwa na tabia ya kushika simu yako mkononi mara kwa muda mrefu huwenda hii ikawa ni moja ya sababu inayo sababisha vidole vyako vya mikono kufa ganzi mara kwa mara. Hakikisha unaweka simu yako mfukoni au kwenye meza pale unapokuwa huitumii.

  • Ugonjwa wa Kupenda Smartphone

Moja kati ya tatizo ambalo watu hudhani sio tatizo ni ugonjwa wa kupenda smartphone, ugonjwa huu umethibitishwa na madaktari na ni moja kati ya tatizo kubwa sana miongoni mwa watumiaji wa simu hizi za kisasa maarufu kama smartphone. Kujua zaidi kuhusu ugonjwa wa kupenda smartphone na dalili zake unaweza kusoma hapa. Kupenda simu kwa muda mrefu kunaweza kusababisha magonjwa mbalimbali ya kiafya na kisaikolojia, kujua zaidi hakikisha unasoma makala hiyo hapo juu.

Na hayo ndio baadhi ya matatizo ya kiafya ambayo unaweza kuyapata kutokana na utumiaji wa simu za mkononi uliopitiliza, kumbuka hakikisha unamuona daktari kama una dalili hizi zinazojirudia mara kwa mara.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use