in

Official Video : Muonekano wa Samsung Galaxy Note 9

Huu ndio muonekano halisi wa simu mpya ya Samsung Galaxy Note 9

Galaxy Note 9

Zikiwa zimebaki siku chache hadi kuzinduliwa kwa simu mpya ya Samsung Galaxy Note 9, Hivi leo kampuni ya Samsung kupitia channel yake ya YouTube imevujisha video yenye kuonyesha muonekano wa simu hiyo pamoja na baadhi ya sifa.

Kama tetesi za simu hii zilivyokuwa zinaonyesha, Samsung inakuja na Pen maalum yenye uwezo wa Bluetooth na hii inaonyesha ndio moja kati ya vitu ambavyo samsung inategemea kuzungumzia sana kwenye uzinduzi wa simu hiyo hapo tarehe 9 mwezi huu.

Mbali na hayo video hii pia inaonyesha kuhusu tetesi za awali za simu hii kuja na ukubwa wa ndani wa GB 512, kwa kuonyesha kuwa simu hii inauwezo wa ukubwa wa Terabyte 1, ambayo hiyo ni kujumlisha ukubwa wa memory card ya GB 512 pamoja na ukubwa wa ndani wa GB 512.

Yote haya tutaenda kuyajua zaidi kwenye uzinduzi wa simu hii mpya ambao utakaofanyika huko Brooklyn, New York City nchini Marekani. Kwa habari zaidi na kuangalia uzinduzi huo mubashara kabisa hakikisha unajiunga nasi kupitia tovuti yetu hapa au kupitia App zetu za mfumo wa Android pamoja na iOS.

Angalia Hapa Mubashara Uzinduzi wa iPhone 14

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.