in

Sony Xperia XZ3 Simu ya Kwanza Kuja na Kamera ya MegaPixel 48

Wote tunajua ubora wa kamera za Sony.. Sasa hii ni zaidi..

Sony Xperia XZ3

Pamoja na kusemekana kuwepo kwa ujio wa simu yenye kamera tisa, Kwa sasa simu zilizopo sokoni zenye kamera kubwa zaidi ni simu za Huawei Porsche Mate RS pamoja na Huawei P20 Pro ambazo zinakuja na kamera zenye uwezo wa Megapixel 40. Wakati kampuni ya Huawei ikiwa imekaa kwa muda mchache kwenye rekodi hiyo, Hivi karibuni Kampuni ya Sony inajiandaa kuchukua rekodi hiyo kwa kuja na simu ambayo ndio itakuwa ya kwanza yenye kamera yenye uwezo wa Megapixel 48.

Sony Xperia XZ3 ndio jina la simu hiyo ambayo hivi leo imeonekana ikiwa kwenye datakazi (Database) ya tovuti ya GFXBench ambayo hutumika kupima uwezo wa simu mbalimbali kabla au hata baada ya kuzinduliwa rasmi. Kwa mujibu wa GSMArena simu hiyo yenye model number H8416 itakuja na mfumo wa Android Oreo 8.0.0, processor yenye uwezo wa Octa Core 2.7GHz pamoja na GPU ya Adreno 630.

Kwa sasa hakuna taarifa zaidi za kuhusu simu hii, ila kwa mujibu wa tovuti mbalimbali simu hii inatarajiwa kuzinduliwa rasmi kupitia mkutano wa IFA 2018 unaotarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi huu hadi tarehe 5 ya mwezi wa nane. Hivi sasa muonekano wa simu hiyo umenukuliwa kuwa unaweza kufanana na picha hizo hapo chini.

Kampuni ya TECNO Yazindua Rasmi Spark 10 PRO

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.