Apps# 13 Jaribu App Hizi Kwenye Simu Yako ya Android (Tanzania)

Jaribu app hizi nzuri za kitanzania kwenye simu yako ya Android
App nzuri za Tanzania App nzuri za Tanzania

Kama wewe ni mfuatiliaji wa tovuti hii lazima utakuwa unajua kuwa, hapa Tanzania Tech tunapata nafasi ya kuangalia App nzuri za Android kila mwezi au pengine kila wiki. Leo kwenye mfululizo wa App nzuri za Android nimekuja na kitu cha tofauti kidogo. Kwenye mfululizo wote wa App nzuri hatujawahi kuzungumzia App nzuri za Tanzania na nadhani ni wakati sasa twende tukajuzane App hizo au wewe unaonaje, utaniambia baadae kwenye maoni hapo chini.

Kumbuka Tanzania Tech na Tanzania Tech Media haijalipwa chochote kuonyesha App hizi, bali hizi ni juhudi binafsi za kukupatia wewe msaada wa kiteknolojia kwa namna moja ama nyingine ili kurahisisha maisha yako ya kila siku kwenye ulimwengu huu wa sayansi na teknolojia. Sasa baada ya kusema hayo twende tuka angalie App hizi nzuri za Tanzania za kuwa nazo kwenye simu yako ya Android.

1. Vsomo

Vsomo
Price: Free

Vsomo ni moja kati ya App ambayo tumesha iongelea sana hapa Tanzania Tech, App hii inakupa uwezo wa kujifunza mafunzo ya ufundi stadi kwa kupitia simu yako ya mkononi. Uzuri zaidi wa App hii ni kuwa App hii inatolewa na VETA hivyo mafunzo yoyote unayoyapata yanatoka kwa wataalam na kizuri zaidi ni kuwa mwisho wa kozi unapewa cheti cha kuhitimu mafunzo uliyo yachukua.

Advertisement

2. MAKATO App

MAKATO App
Price: Free

Makato App hii ni App nzuri na ni moja kati ya App ambayo mimi binafsi naitumia, App hii ina kupa msaada wa kuonyesha makato mbalimbali utakayo katwa wakati wa kufanya miamala mbalimbali ya fedha, App hii inakuruhusu kuweka kiasi na baada ya hapo utaweza kuona kiasi cha makato utakayo katwa.

3. Mawazo ya Biashara

Mawazo ya Biashara
Price: Free+

Mawazo ya Biashara ni App nyingine nzuri sana kufuatilia, Japo kuwa bado hatutajua taaluma ya mtu mwenye App hii lakini ni wazi kuwa App hii ina mawazo mengi sana mazuri kwa mtu yoyote anayetaka kufanya biashara. App hii ni nzuri kwa wafanya biashara wote wanao anza hata wale wanao endelea.

4. Vocha Master

Vocha Master ni App nyingine nzuri ya Android App hii itakusaidia kuingiza vocha kwenye simu yako kwa urahisi, App hii itakusaidia kuingiza vocha kwa ku-scan vocha yako na utaweza kuiweka kwenye simu yako kwa haraka zaidi.

5. Shule Direct

Shule Direct
Price: Free

Shule Direct ni App nyingine nzuri sana kwa ajili ya wanafunzi na walimu, App hii inakusaidia wewe kama mwanafunzi kujifunza masomo mbalimbali kwa kupitia simu yako ya mkononi. Vilevile App hii ina nafasi ya walimu kwa ajili ya kuweza kutoa masomo mbalimbali kwa ajili ya wanafunzi.

6. Kilimo Na Ufugaji Bora

Kimo bora na ufugaji ni App nzuri sana kwa wale watu waliojikita katika fursa za kilimo na ufugaji, kupitia App hii utaweza kujifunza mambo mbalimbali kuhusu kilimo bora pamoja na ufugaji kwa hapa Tanzania.

7. SomaApp : Free Scholarships, Paid Internships.

Soma App ni app nyingine nzuri ambayo inakupa, fursa ya elimu kwa kupata uzamini wa kimasomo Mikutano, Ushirikiano, Warsha kazi za muda mfupi pamoja na mambo mengine mbalimbali yanayo husiana na elimu kwa mwanafunzi wa kiafrika.

8. Herufi na Akili – Akili and Me

  • Kiswahili
  • Kiingereza

Kama wewe una mtoto au unaye mdogo wako basi app hii ni nzuri sana kuweza mfundisha baadhi ya mambo kuhusu kusoma. App hii ni nzuri sana na kama unahitaji mwanao aweze kujifunza kusoma kwa haraka basi jaribu app hii.

App bado nyingi sana na bado tunaendelea kupokea maoni ya app nyingine nzuri za kitanzania. Unaweza kutoa maoni ni App gani nzuri ya kitanzania unayo tumia au kama wewe ni mbunifu wa programu mbalimbali unaweza pia kutumia jina la App yako na sisi tutaiweka hapa kwa ajili ya watanzania wote. Unaweza kusoma hapa kujua app nyingine nzuri za kutumia kwenye simu yako ya Android.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use