in

Sasa Angalia Video za Instagram na Facebook Ndani ya WhatsApp

Sasa utakuwa na uwezo wa kuangalia video ndani ya Whatsapp

WhatsApp-iOS

WhatsApp imekuwa ikifanya maboresho ya programu yake kila siku, Maboresho haya mengi yamekuwa yakiangalia zaidi watumiaji wa programu ya WhatsApp ya mfumo wa Android, lakini sasa hali hii imebadilika kwani hivi karibuni watumiaji wa programu ya WhatsApp ya mfumo wa iOS wataenda kufurahia sehemu mpya kadhaa zinazokuja kwenye programu ya WhatsApp.

Moja ya sehemu hizo ni pamoja na uwezo wa kuangalia video za mtandao wa Instagram na Facebook ndani ya programu ya WhatsApp. Sehemu hii inafanya kazi pale mtu atakapo kutumia Link ya video ya mtandao wa Facebook au Instagram utaweza kuangalia video hiyo moja kwa moja ndani ya Programu ya WhatsApp bila kutoka nje ya programu hiyo.

Kama ilivyo kwenye video za Youtube sasa hata video za Instagram pamoja na Facebook zitaweza kuonyesha ndani ya programu ya WhatsApp kama inavyo onekana kwenye video hapo juu. Kwa watumiaji wa programu ya WhatsApp ya Android, sehemu hii haipo na bado hakuna taarifa lini sehemu hii itakuja rasmi kwenye simu zenye mfumo wa Android.

Apps (7) za Muhimu Kuwa Nazo Kwenye Android TV (2022)

Kama unatumia simu yenye mfumo wa iOS basi unaweza kusasisha toleo jipya la programu ya WhatsApp kupitia App Store kisha jaribu sehemu hiyo kisha tuambie maoni yako hapo chini.

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

2 Comments