in

Kampuni ya Xiaomi Yazindua Simu Mpya ya Xiaomi Redmi S2

Simu hii inakuja na mfumo wa AI kwenye kamera yake ya mbele

Xiaomi Redmi S2

Kampuni ya Xiaomi hivi karibuni imerudi tena na toleo jipya la simu yake ya Xiaomi Redmi S2, simu hii inakuja na muonekano kama wa simu ya Xiaomi Redmi Note 5 ambayo yenyewe ni maalumu kwa nchini China. Simu ya Xiaomi Redmi S2 yenyewe inaendeshwa na processor ya Snapdragon 625 chipset, CPU ya octa-core yenye uwezo wa 2.0 GHz ikiwa pamoja na GPU ya Adreno 506 GPU.

Mbali na sifa hizo, simu hii inakuja na mfumo wa AI au Artificial intelligence kwenye kamera yake ya mbele ambayo itakusaidia kuchukua picha nzuri za selfie kwenye mwanga mdogo pamoja na picha za portrait, sifa nyingine za Xiaomi Redmi S2 ni kama zifuatazo.

Sifa za Xiaomi Redmi S2

 • Ukubwa wa Kioo  – Inch 5.99 chenye teknolojia ya IPS LCD display, chenye uwezo wa kuonyesha rangi milioni 16 pamoja na resolution ya 720 x 1440 pixels, 18:9 ratio (~269 ppi density).
 • Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.1 (Oreo)
 • Uwezo wa Processor – Octa-core 2.0 GHz Cortex-A53, Qualcomm MSM8953 Snapdragon 625 Chipest.
 • Uwezo wa GPU – Adreno 506
 • Ukubwa wa Ndani – Ziko simu za aina mbili moja itakuwa na GB 32 na nyingine itakuwa na uwezo wa GB 64 zote zikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 256.
 • Ukubwa wa RAM – Ziko simu za aina mbili moja itakuwa na RAM ya GB 3 na nyingine itakuwa na RAM ya GB 4.
 • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 16 yenye (2.0µm), HDR, LED flash.
 • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko Mbili moja ina Megapixel 12 yenye uwezo wa (f/2.2, 1.25μm, PDAF) na nyingine yenye Megapixel 5 zote zikiwa na uwezo wa gyro-EIS, phase detection autofocus, LED flash.
 • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Po 3080 mAh Battery
 • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bletuooth 4.2, A2DP, LE pamoja na GPS ya A-GPS, GLONASS, Tyep C USB.
 • Rangi – Inakuja kwa rangi tatu za Rose Gold, Champagne Gold na Platinum Silver
 • Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Micro-SIM, dual stand-by) , inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
 • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G.
 • Ulinzi – Inayo Fingerprint. (Kwa Nyuma)
Kampuni ya Airtel ya Kwanza Kuja na eSIM Tanzania

Kwa upande wa bei simu ya Xiaomi Redmi S2 ya GB 32 na RAM ya GB 3 itauzwa kwa Yuan ya China CNY999 sawa na Tsh 360,000 na kwa upande wa Xiaomi Redmi S2 ya GB 64 na RAM ya GB 4 yenyewe itauzwa kwa Yuan ya China CNY1,299 sawa na Tsh 467,000. Simu zote hizi kwa sasa zinapatikana nchini china na bado hakuna taarifa kuhusu simu hizi kuja nchi nyingine.

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

One Comment