Samsung Kuja na Toleo Jipya la Samsung Galaxy S8 Lite

Simu hii inatarajiwa kuzinduliwa mwezi huu tarehe 27 mwezi may
Galaxy S8 Lite Galaxy S8 Lite

Kampuni ya Samsung imekua ikizindua simu nyingi bila hata kutangaza rasmi kwa wateja wake, Hivi karibuni Samsung imetangaza ujio wa simu mpya za Galaxy A6 pamoja na A6 Plus (2018). Lakini kama haitoshi inasemekana kuwa Samsung inatarajia kuzindua toleo jipya la simu ya Galaxy S8 Lite.

Kwa mujibu wa tovuti ya GSM Arena, Galaxy S8 Lite inatarajiwa kuzinduliwa mwezi huu huko nchini China na simu hiyo inasemekana kuja na muundao kama wa Galaxy S8 kama inavyo onekana kwenye picha hapo chini.

Kwa mujibu wa tovuti hiyo Galaxy S8 Lite, itakuja na processor ya Snapdragon 660 ambayo inasaidiwa na RAM ya GB 4 pamoja na ukubwa wa ndani wa GB 64. Simu hii pia inakuja na kioo cha inch 5.8 kama ilivyo Galaxy S8 ya kawaida lakini tofauti itakuwa kwenye resolution ambayo itakuwa ni 1080 x 2220 pixel. Kwa upande wa battery simu hii itakuwa na battery inayo fanana na S8 ambayo itakuwa na uwezo wa Li-Ion 3000mAh.

Advertisement

Tetesi hizo zinasema kuwa simu hiyo inategemewa kuzinduliwa tarehe 27 mwezi huu wa tano na inategemewa kuzinduliwa kwa nchini China. Kwa sasa bado hakuna taarifa zaidi kama simu hii itakuja nchi nyingine mbalimbali duniani. Kujua zaidi endelea kutembelea Tanzania Tech.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use