in

Samsung Kuzindua Simu Mpya ya Galaxy J6 (2018) May 21

Simu hii inatrajiwa kuja na kioo cha kisasa cha Infinity Display

Galaxy J6 (2018)

Kampuni ya Samsung imetuma mialiko kwa kampuni mbalimbali kuhudhuria tamasha la uzinduzi wa simu zake mpya. Kwa mujibu wa tovuti ya Gadget 360 tamasha hilo litakuwa linahusu uzinduzi wa simu mpya za Samsung Galaxy J6 (2018) pamoja na matoleo mapya ya Galaxy A Series.

Kwa mujibu wa tovuti hiyo, baadhi ya picha tayari zimesha vuja zikionyesha muonekano wa simu hizo mpya za Galaxy J6 (2018), na hapo chini ndio picha hizo ambazo zinasemekana ndio muonekano halisi wa Galaxy J6 (2018).

Hata hivyo simu hii ya Galaxy J6 (2018) inatarajiwa kuuzwa kwa Euro €250 ambayo ni sawa na Tsh 674,000 sifa za simu hii bado hazijajulikana rasmi ila endelea kutembelea Tanzania Tech tutakujuza kuhusu sifa za simu hii ikiwa pamoja na kuonyesha tamasha hilo mubashara kabisa.

Kwa sasa tayari kampuni ya Samsung imesha zindua simu hii mpya ya Galaxy J6 (2018), Kama unataka kujua bei na sifa kamili za simu hii unaweza kusoma hapa kuzijua sifa kamili za Galaxy J6 (2018).

Usinunue Simu ya Android au iPhone ya Zamani

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.