Mark Zuckerberg Kuhojiwa Kesho na Wabunge wa Ulaya

Mark Zuckerberg kujibu maswali ya wabunge wa ulaya kesho
mark-zuckerberg kuhojiwa ulaya mark-zuckerberg kuhojiwa ulaya

Mwaka huu 2018 umekuwa ni mwaka wa tofauti kidogo kwa kampuni ya Facebook pamoja na mkurugenzi wake Mark Zuckerberg, hata hivyo hali hiyo imechagizwa na kushutumiwa kwa Facebook kufanya uzembe ulio sababisha uvujishaji wa data za mamilioni ya watumiaji wa mtandao huo kwenye kipindi cha uchaguzi wa Raisi wa marekani mwaka 2016.

Hata hivyo Facebook imefanya mabadiliko makubwa kwa watumiaji wake ikiwa pamoja na kuweka vigezo na masharti makali juu ya wabunifu mbalimbali wa programu na tovuti wanaotumia mtandao huo kwa namna mbalimbali. Japokuwa Facebook imefanya mabadiliko hayo bado baadhi ya viongozi mbalimbali wa nchi za ulaya bado wana mashaka juu ya data za wananchi wake kitendo ambacho kinafanya Mark Zuckerberg kuhojiwa tena na wabunge wa ulaya hapo kesho.

Kwa mujibu wa tovuti ya The Verge, Mark Zuckerberg atahojiwa na wabunge wa ulaya mubashara kabisa na itakuwa inaonyeshwa rasmi kupitia Tovuti ya Bunge la Ulaya kuanzia saa 2:15 usiku (saa mbili na robo usiku) hadi saa 3:30 usiku (saa tatu na nusu usiku) kwa saa za Afrika Mashariki.

Advertisement

Kwa mujibu wa Tweet iliyotolewa na Rais wa Bunge la Ulaya, Antonio Tajani Mark Zuckerberg amekubali mahojiano hayo kuonyeshwa mubashara baada ya Raisi huyo wa bunge la ulaya kuongea na Mark Zuckerberg akimtaka kuruhusu tukio hilo kuonyeshwa mubashara kupitia tovuti ya bunge la ulaya hapo kesho.

Tanzania tech tutajitahidi kuleta mahojiano hayo mubashara kupitia hapa hapa Tanzania Tech, endelea kutembelea tovuti hii ili kupata habari zaidi jinsi tukio hilo litakavyokuwa pamoja na habari zaidi kuhusu Facebook na teknolojia kwa ujumla.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use