in

Instagram Kuja na Njia Mpya ya Kunyamazisha (Mute) Picha za Mtu

Utaweza kunyamazisha picha na Stories za mtu yoyote

instagram mute

Mtandao wa Instagram hivi karibuni umeonekana ukifanya majaribio ya sehemu mpya ya “MUTE”, sehemu hii inaleta uwezo wa Kunyamazisha picha au post mbalimbali za watu zisionekana kwenye timeline yako kwenye mtandao wa Instagram. Yaani badala ya kum-unfollow mtu sasa utaweza kunyamazisha au ku-mute picha za mtu huyo na hazito weza kuonekana kwenye sehemu yako ya timeline.

Mbali na hayo sehemu hii inakupa uwezo wa kunyamazisha au ku-mute picha au Stories za mtu huyo, au unaweza kunyamazisha stories na picha kwa pamoja. Hata hivyo kwa mujibu wa ripoti kutoka tovuti ya The Verge, Instagram inasema kuwa sehemu hii ni bora zaidi kuliko kum-unfollow mtu, kwani pale utakapo nyamazisha picha au stories za mtu fulani yeye hatoweza kujua na pia utakuwa na uwezo wa kuwasha au ku-unmute picha na stories za mtu huyo muda wowote.

Sehemu hii mpya ya Mute inategemea kuja kwenye instagram wiki za karibuni kupitia simu za mifumo yote ya Android pamoja na iOS. Japokuwa unaweza kum-unfollow mtu pale utakapo kuwa hutaki kuona post au picha zake, je unadhani sehemu hii ina umuhimu kuwepo kwenye mtandao wa Instagram..? Tuambie kwenye maoni hapo chini.

Apps Nzuri za Kufuatilia kwa Karibu Kombe la Dunia

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.