Jinsi ya Kuangalia Kama Cambridge Analytical Ilitumia Data Zako

Utaweza kujua kama data zako zilitumiwa kwa namna yoyote na kampuni hiyo
kampuni ya cambridge-analytica-facebook kampuni ya cambridge-analytica-facebook

Wakati hivi leo Mwenyekiti na mkurugenzi mtendaji wa Facebook Mark Zuckerberg, yuko kwenye awamu ya kwanza ya mahojiano na seneti ya marekani kuhusu sakata la Cambridge Analytical, hivi leo Facebook imetoa njia ya kuweza kujua kama data zako za siri zilitumika na Cambridge Analytical kwa namna yoyote.

Kupitia ukurasa wa Facebook wale walio adhiriwa na uwizi huo wa data, wanategemewa kutumiwa ujumbe maalum ambao utawataka kujua kuwa data zao au za marafiki zao zilitumika na mtandao huo. Hata hivyo kama hujapokea ujumbe huo unaweza kuangalia kama data zako za siri zilitumika kwa kufuata njia hii rahisi hapo chini.

Unachotakiwa kufanya ni kutembelea UKURASA HUU, ukiwa umeingia kwenye akaunti yako ya Facebook kisha soma maelezo ambayo yatakuwa kwenye ukurasa huo. Kwa namna hiyo kama umeadhiriwa facebook kupitia ukurasa huo itapendekeza ubadilishe (settings) mpangilio wa programu zenye uwezo wa kubadilisha vitu kwenye ukurasa au akaunti yako ya Facebook.

Advertisement

Kama unataka uhakika zaidi unaweza kutembelea UKURASA HUU, ukiwa umeingia kwenye akaunti yako ya Facebook na utaona kila programu yenye uwezo wa kubadilisha vitu kwenye ukurasa wako wa Facebook. Unaweza kubadilisha au kondoa uwezo wa programu hizo kupitia ukurasa huo.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use