in

Rihanna Aituhumu Snapchat kwa Sababu ya Tangazo Lao

Amesema kuwa Snapchat sio mtandao anao upenda zaidi

Rihanna Aituhumu Snapchat kwa Sababu ya Tangazo Lao

Weekend hii sakata jipya limeibuka mtandaoni baina ya mwanamzuiki maarufu kutoka marekani Rihanna, pamoja na mtandao maarufu wa Snapchat. Sakata hilo limekuja baada ya Snapchat kuruhusu kuweka tangazo la mchezo au Game, ambapo tangazo hilo liliwataka watumiaji wa mtandao kuchagua jibu moja kwenye picha kupitia game hiyo.

Tangazo hilo ambalo linatolewa na game maarufu ya Would You Rather, lilimuweka mwanamuziki Rihanna pamoja na mwanamuziki mwingine Chris Brown ambao walishawahi kuwa wapenzi. Sasa tatizo halipo kwenye picha hizo kuwekwa pamoja, bali kwenye picha hizo unatakiwa uchague chaguo moja gumu huku maneno yakiwa yameandikwa “utachagua umpige nani kati ya wawili hao kwenye picha hiyo” ikiwa ni lazima uchague mmoja kati ya wawili hao.

Sasa kupitia ukurasa wake wa Instagram, Rihanna aliwatuhumu snapchat kwa kuruhusu picha hiyo isiyo na maadili huku ikiituhumu Snapchat kuwa inasisitiza unyanyasaji wa kijinsia kwa kuruhusu Tangazo hilo. Rihanna alisema kuwa hata hivyo Snapchat sio mtandao anao upenda zaidi huku akiita kitendo hicho cha kuruhusu tangazo hilo ni kitendo cha kijinga.

Snapchat kupitia mitandao mbalimbali ilitangaza kuomba msamaa juu ya kuruhusu tangazo hilo na kusema kuwa, tangazo hilo liliruhusiwa kwa bahati mbaya na kusema kuwa imeondoa tangazo hilo na inafuatilia kwa undani zaidi ili kujua jinsi tukio hilo lilivyo tokea na kuhakikisha kuzuia isitokee tena kwa siku za mbeleni.

Fahamu Yote ya Muhimu Kuhusu Mfumo wa Android 13

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.