in

IBM Yazindua Kompyuta Ndogo Kuliko Zote Duniani

Fahamu hii hapa ndio kompyuta ndogo kuliko zote duniani

IBM Yazindua Kompyuta Ndogo Kuliko Zote Duniani

Kampuni ya utengenezaji wa kompyuta pamoja na vifaa mbalimbali vya kieletroniki ya IBM yenye makao yake makuu huko Armonk North Castle nchini marekani, hivi karibuni imetangaza ujio wa kompyuta ndogo kuliko zote duniani.

Kompyuta hiyo ambayo ni ndogo kama punje ya chumvi, imezinduliwa hivi karibuni kwenye mkutano wa kampuni hiyo unaojulikana kama IBM Think 2018. Kwa mujibu wa mitandao mbalimbali kompyuta hiyo ni ndogo sana kiasi kwamba unahitaji kifaa cha maabara maarufu kama microscope ili uweze kuiona kompyuta hiyo.

Kama inavyo onekana kwenye picha hapo juu, kompyuta hiyo ni ndogo kiasi kwamba ikilinganishwa kwenye chembe za chumvi, bado inakuwa ni ngumu kuweza kuiona kwa macho ya kawaida.

Kujua ukubwa wake kabisa, kompyuta hii inakubwa wa size ya 1x1nm ambao ni size ndogo kuliko hata punje ya mchele. Kwa upande wa uwezo kompyuta hii ina nguvu sawa na kompyuta zenye mfumo wa x86 na imetengenezwa kwaajili ya kufanya kazi mbalimbali ikiwa pamoja na kazi za mfumo wa Artificial Intelligence au (AI) pamoja na kazi zingine kama kugundua uwizi, usafirishaji na mambo mengine kama hayo.

Jinsi ya Kupunguza Mwanga wa Kompyuta (Njia Bora Sana)

Kutokana na udogo wa kompyuta hiyo, kampuni ya IBM imesema ina matumaini makubwa kuwa kompyuta hiyo itaanza kutumika ndani ya simu janja mbalimbali kwenye miaka ya karibuni.

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

2 Comments