Waziri Mkuu Tanzania Ameagiza Viwanda Kutumia Barcodes za GSI

Viwanda Nchini Tanzania Kuanza Kutumia Barcodes za GSI
G1 Barcode G1 Barcode

Taarifa kutoka idara ya habari maelezo hapa nchini Tanzania zinasema kuwa, WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameagiza kila kiwanda kilichopo nchini kihakikishe kinatumia alama za utambuzi za GS1 Tanzania simbomilia au Barcodes.

Magizo hayo yametolewa siku ya jana Alhamisi, Februari 22, 2018 wakati waziri mkuu akifungua Mkutano wa Sita wa Wamiliki wa Viwanda na Watumiaji wa simbomilia au (Barcodes). Kwa mujibu wa tovuti ya wizara ya habari ya Tanzania, waziri mkuu alisema “Natoa wito kwa wenye viwanda kutumia GS1 Tanzania kutangaza na kuuza bidhaa zenye ubora katika maduka ya kimataifa, ambapo pia bidhaa zao zitachangia katika ulipaji wa kodi kwa usahihi”.

Hata hivyo Waziri Mkuu amesema kuwa barcodes ni muhimu sana kwa sababu zinawawezesha wajasiriamali nchini kuuza bidhaa zao katika maduka rasmi ya nje na ndani ya Tanzania. Amesema kuwa, miaka ya nyuma kabla ya kuanzishwa kwa GS1 Tanzania, wazalishaji wa bidhaa za Tanzania walilazimika kwenda nje ya nchi yetu kutafuta barcodes ili waweze kuuza bidhaa zao.

Advertisement

Waziri mkuu aliendelea kusema kuwa hali hiyo iliifanya Tanzania kuwa wategemezi na kuchangia kuzalisha ajira kwa ajili ya nchi nyingine kwa kununua barcodes zao. “Tangu kuanzishwa kwa chombo chetu, tumejinasua kutoka katika utegemezi huo.

Pia Waziri Mkuu amesema amefurahishwa na mipango iliyowekwa na GS1 Tanzania ya kuhakikisha kwamba mazao ya kilimo yanapatiwa barcodes na kuwaelimisha wananchi kuhusu alama hizo.

Mkutano huo umehudhuriwa na Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhandisi Stella Manyanya, Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara SMZ, Balozi Amina Salum Ally, Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof. Elisante Ole Gabriel.

Wengine walio hudhuria mkutano huo hapo jana ni Mwenyekiti wa Bodi ya GS1 Tanzania Dkt. Gidion Mazara, Wakuu wa Taasisi na Wadau wa GS1 kutoka Tanzania Bara na Visiwani (TBS, BRELA, TANTRADE, ZNCIAAL, COSTECH na Mtendaji Mkuu wa GS1 Tanzania Bi. Fatuma Kange

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use