Mabasi Mapya 70 ya Mwendokasi Yapokelewa Dar es Salaam

Mabasi haya mapya yanauwezo wa kuchukua abiria wengi zaidi
mabasi ya mwendokasi mabasi ya mwendokasi
Picha na AzamTV

Hivi karibuni, Kampuni ya mabasi yaendayo haraka (UDART) imepokea mabasi mapya 70 yenye uwezo wa kubeba abiria zaidi ya 100 tofauti na magari ya awali yaliyoletwa katika awamu ya kwanza ya mradi wa huo

Taarifa kutoka kwenye mtandao wa Azamtv zinasema kuwa, mabasi hayo yamepokelewa katika Bandari ya Dar es Salaam ambapo inasemekana ujio wa mabasi hayo utaongeza ufanisi zaidi katika kutoa huduma pamoja na kuzalisha ajira mpya hapa jijini dar es salaam.

Katika upokeaji wa mabasi hayo siku chache zilizopita mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya (UDART), Charles Nawe amesema, tofauti ya ubora uliopo kati ya mabasi hayo mapya na ya awali ni muundo wa mabasi hayo pamoja na uwezo wa kuchukua abiria wengi kwa wakati mmoja.

Advertisement

Hata hivyo kwa mujibu wa mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya magari yaendayo haraka UDART Charles Nawe aliye ongea na Azamtv, alisema kuwa mabasi hayo yataendelea na safari za barabara zilizopo sasa hadi pale watakapo anzisha barabara nyingine zinazo tegemewa kuanzishwa miaka ya karibuni.

Mpaka sasa inasemekana Kampuni ya UDART ina jumla ya mabasi ya mwendokasi takribani 210 huku maitaji yakiwa ni takribani mabasi 305 kwa jijini dar es salaam.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use