in

Mwanamuziki Chamillionaire Azindua App Yake Mpya ya Convoz

Sasa utaweza kuchati na Wasani Unao wapenda kupitia Video

Chamillionaire na App ya Convoz

Mwanamuziki ambae ni rapper wa zamani kidogo wa nchini marekani Chamillionaire, hivi karibuni amezindua App yake mpya inayoitwa Convoz. App hiyo mpya ambayo itahusiana na mitandao ya kijamii ni moja kati ya App ya tofauti sana.

Akiwa kwenye mkutano wa uzinduzi wa App hiyo, ambao pia ulikua mkutano wa wawekezaji na wajasiriamali, mwanamuziki Chamillionaire alitangaza kuhusu App hiyo mpya ya Convoz ambayo ita kuwa ikiunganisha watu mbalimbali kwa njia ya video kama ilivyo stories.

https://www.instagram.com/p/BXWQRuBFdqV/?utm_source=ig_embed

Lakini tofauti na Stories iliyopo kwenye App nyingi za sasa za mitandao ya kijamii, App ya Convoz inashirikisha mastaa na wasanii mbalimbali ambao unaweza kuongea nao moja kwa moja kupitia video ndani ya App hiyo.

Tofauti na kuchat kwa maneno ya kuandika, kupitia App hiyo mpya ya Convoz utaweza kuchati kwa kutumia video na ili kutumia app hiyo mtumiaji anakuwa na uwezo wa kurekodi video na kisha kuituma kwa msanii au mtu yoyote anaye mpenda alafu baadae msanii huyo hujibu meseji hiyo na yote hayo hufanyika kwa njia ya Video.

Apps za Kusaidia Kujibu Meseji WhatsApp (Bila Kushika Simu)

Kwa sasa App hii bado haija anza kupatikana rasmi Tanzania, lakini kupitia tamasha la uzinduzi wa App hiyo (Upfront Summit in Los Angeles), Chamillionaire ameahidi kufikisha App hiyo kila upande duniani na hii ni kutoa nafasi kwa watu kuweza kuongea na kuwaona wasanii na watu wanao wapenda.

Kwa sasa App hiyo inapatikana nchini marekani na ili kujua siku itakapo fika Tanzania unaweza kuendelea kutembelea Tanzania Tech au kutembelea ukurasa huu na kujaribu kubofya link hapo chini.

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.