in

Galaxy S8 na S8+ Kupata Toleo la Android 8.0 Oreo Mwezi Huu

Baada ya majaribio kukamilika Sasa watumiaji wa S8 kupata Android 8.0 Oreo

Smaung Galaxy S8 Android 8.0 Oreo

Hadi kufikia mwezi December mwaka jana 2017, asilimia 0.5% pekee ya watumiaji wa simu za Android ndio walikuwa wanatumia simu zenye toleo jipya la Android 8.0 Oreo, asilimia hizi zinaenda kubadilika na kuongezeka kwa sababu sasa kampuni ya samsung ipo tayari kutoa toleo hilo jipya la Android kwa watumiaji wa simu za Samsung Galaxy S8 pamoja na S8 Plus.

Kwa mujibu wa kampuni ya Samsung majaribio ya toleo hilo la Android 8.0 Oreo kwenye simu za Samsung Galaxy S8 na S8 Plus yame fanikiwa vizuri na yana tegemewa kukamilika ifikapo tarehe 17 mwezi huu. Hata hivyo kampuni hiyo pia imesema ndani ya mwezi huu ina tegemewa kuanza kutoa toleo hilo jipya la Android Oreo 8.0 kwenye simu za Galaxy S8 pamoja na S8 Plus.

Vilevile Samsung imetangaza kuwa toleo hilo jipya litakuja na maboresho mengi sana ikiwemo muonekano mpya wa Samsung Experience 9.0 pamoja na maboresho mengine mengi. Kwa sasa bado haijajulikana tarehe kamili ya kutoka kwa toleo hilo lakini watumiaji wote wa simu hizo wanategemea kuanza kupata toleo hilo kabla ya kuisha kwa mwezi huu.

Kujua lini toleo hili litakufikia, endele kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kupata habari mpya kwa kupakua App yetu mpya ya Tanzania Tech kupitia soko la Play Store. Bila kusahau kama unataka kujifunza maujanja mabambali basi unaweza kutembelea Channel yetu ya Tanzania Tech kupitia mtandao wa Youtube.

Usinunue Simu za Zamani Zenye Umri Zaidi ya Miaka 4

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.