in

YouTube Kuja na Huduma Mpya ya Kusikiliza Muziki Mwaka 2018

Wasanii na Wanamuziki Yajiandae kunufaika na huduma mpya ya Muziki

Huduma mpya za music YouTube

Pamoja na mtandao wa Youtube kuwa mtandao muhimu kwa wasanii na wanamuziki, lakini kampuni ya Google imeona bado haitoshi. Ripoti kutoka mtandao wa Bloomberg zinasema kuwa, youtube kwa sasa inajipanga kuja na huduma mpya ya kusikiliza muziki (music live streaming) ifikapo mwaka 2018.

Huduma hiyo inayo tegemewa kuanza mwanzoni au katikati ya mwaka 2018 itakuwa ikifanana na huduma nyingine za muziki kama Spotify, Apple Music na nyingine kama hizo.

Pamoja na kuwa Youtube tayari inayo huduma za muziki za kulipia kama vile Youtube Red na Youtube Music huduma ambazo bado hazijafika Tanzania, lakini Google imepaga kufanya huduma hiyo mpya ya kusikiliza muziki kuwa bora zaidi.

Hapo mwaka jana YouTube ilimuajiri mkurugenzi mtendaji wa zamani wa kampuni ya Warner Music Lyor Cohen, ambae alijiriwa kwaajili ya kusimamia maswala mazima ya muziki na kwa mujibu wa mtandao wa Bloomberg, Lyron alitangaza ujio wa huduma mpya za muziki.

Je nini maoni yako kwenye hili.. Unadhani huduma hizo mpya za YouTube kwaajili ya kusikiliza muziki zitafanikiwa kwa kiwango kikubwa kama zilivyo huduma za Spotify na Apple Music..? Tuambie maoni yako hapo chini.

Video : Angalia Uzinduzi wa MacBook Mpya Kwa DK 10

Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha una download App yetu mpya ya Tanzania Tech kupitia Play Store na vilevile tembelea channel yetu ya Tanzania Tech kupitia Youtube ili uweze kujifunza zaidi mambo yote ya teknolojia kwa njia ya Video.

Amani Joseph

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Avatar

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.