in

Watumiaji 10 wa YouTube Wanaolipwa Hela Nyingi (2017)

Hii ndio list ya watumiaji wa mtandao wa Youtube wanaolipwa hela nyingi zaidi

Pesa Nyingi Youtube

YouTube ni mtandao wa kijamii ambao pengine ndio mtandao wa kwanza unaowalipa watumiaji wake kwa kuweka video za makala mbalimbali kwenye akaunti zao kupitia mtandao huo.

YouTube kupitia kampuni ya Google imekua inafanya hivyo kwa watumiaji wake kutokana na matangazo yanayopitishwa kwenye makala hizo za video hii kusababisha Youtube kupata mapato ambayo yanagawanywa kwa mtu mwenye video pamoja na kampuni yenyewe yaani Youtube.

Mpaka sasa tayari mtandao huu umesha toa mamilioni ya dollar za kimarekani kwa watumiaji wake na hii ni tofauti kwa kila mwenye akaunti kutokana na aina ya matangazo pamoja na inchi uliyoipo, bila kusahau aina ya video uliyotuma na idadi ya watu walio angalia video yako.

Najua unajiuliza lakini yapo mambo mengi sana ya kuzingatia ili kuwa na kipato kikubwa kwenye mtandao huo, tufanye hiyo ni topic ya siku nyingine lakini kwa leo hebu tuangali list ya watumiaji kumi 10 wa mtandao huu wa youtube wanaolipwa hela nyingi zaidi kutokana na mtangazo yanayopita kwenye video zao.

Kumbuka matokeo haya yanatoka kwenye mtandao wa Social Blade na yanaweza kubadilika muda wowote lakini kwa sasa hawa ndio watumiaji wa mtandao huo wanaolipwa pesa nyingi zaidi.

10Colleen Ballinger

 • YouTube Channel – PsychoSoprano
 • Subscribers – Milioni 5,283,844
 • Kiasi cha Dollar za Marekani Milioni $5 kwa mwaka sawa na Tsh 11,269,500,000

9. Rhett & Link

 • YouTube Channel – Rhett & Link
 • Subscribers – Milioni 4,382,548
 • Kiasi cha Dollar za Marekani Milioni $5 kwa mwaka sawa na Tsh 11,269,500,000

8. German Garmendia

 • YouTube Channel – HolaSoyGerman
 • Subscribers – Milioni 32,615,006
 • Kiasi cha Dollar za Marekani Milioni $5.5 kwa mwaka sawa na Tsh 12,396,450,000

7. Markiplier

 • YouTube Channel – Markiplier
 • Subscribers – Milioni 18,720,777
 • Kiasi cha Dollar za Marekani Milioni $5.5 kwa mwaka sawa na Tsh 12,396,450,000

6. Tyler Oakley

 • YouTube Channel – Tyler Oakley
 • Subscribers – Milioni 7,902,534
 • Kiasi cha Dollar za marekani Milioni $6 kwa mwaka sawa na Tsh 13,523,400,000

5. Rosanna Pansino

 • YouTube Channel – Rosanna Pansino
 • Subscribers – Milioni 9,157,795
 • Kiasi cha Dollar za marekani Milioni $6 kwa mwaka sawa na Tsh 13,523,400,000

4. Smosh

 • YouTube Channel – Smosh
 • Subscribes – Milioni 22,751,842
 • Kiasi cha Dollar za marekani Milioni $7 kwa mwaka sawa na Tsh 15,777,300,000

3. Lilly Singh

 • YouTube Channel – IISuperwomanII
 • Subscribes – Milioni 12,614,925
 • Kiasi cha Dollar za marekani Milioni $7 kwa mwaka sawa na Tsh 15,777,300,000

2. Roman Atwood

 • YouTube Channel – RomanAtwoodVlogs
 • Subscribes – Milioni 13,774,031
 • Kiasi cha Dollar za marekani Milion $8 kwa mwaka sawa na Tsh 18,031,200,000

1. PewDiePie

 • YouTube Channel – PewDiePie
 • Subscribes – Milioni 57,857,091
 • Kiasi cha Dollar za marekani Milion $15 kwa mwaka sawa na Tsh 33,808,500,000

Na hiyo ndio list ya watumiaji wa mtandao wa Youtube wanaolipwa hela nyingi kwa sasa, kumbuka list hii ilichapishwa rasmi tarehe September 14, 2017 na makadirio ya data zote hizo ni kwa mujibu wa tovuti ya Social Blade

Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha una download App ya Tanzania Tech kupitia Play Store pia usasahau kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech kupitia Youtube ili uweze kupata habari zote za teknolojia kwa njia ya Video.

WhatsApp Kuacha Kufanya Kazi Kwenye Simu Hizi (November)

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

4 Comments

 1. Najitahidi sana lakini bado watazamaji wa video zangu huwa wachache sana sijuwi kwa nini naomba msaada zaidi,kuna njia gani za kufanya video iwe na watazamaji weeengi!!kama za wengine!!au kuna sehemu ya kuwa unalipia!!!