in

Facebook Yaja na “Facebook Creator” App Mpya Kwaajili ya Video

Njia mpya ya kuweza kufurahia utengenezaji wa Video kupita Facebook

facebook creator

Katika jitihada za kushindana na mtandao wa Youtube hivi, karibuni kampuni ya facebook imetangaza ujio wa App yake mpya inayoitwa “Facebook Creator”. App hii imetengenezwa rasmi kwaajili ya  watengenezaji wa video pamoja na wapenzi wa video kwa ujumla.

Programu hiyo mpya inakuja na vitu mbalimbali ndani yake ikiwemo vitu vitakavyo kusaidia kutengeneza video kwa urahisi zaidi, ikiwa pamoja na kutengeneza utangulizi wa Video, kuweka stika kwenye video pamoja na kutengeneza picha au video kwaajili ya sehemu ya Stories.

Vilevile App hiyo itakusaidia kurekodi video mubashara (Live Video) pamoja na kukupa njia za kuwasiliana kupitia mtandao wa instagram pamoja na Facebook Messenger. “Facebook Creator” itakupa pia uwezo wa kuona matokeo mbalimbali ya idadi ya watu walio angalia video zako ikiwa pamoja na idadi ya watu walio tembelea ukurasa wako kwa ujumla.

Kwa sasa App ya Facebook Creators inapatikana kupitia mfumo wa iOS pekee, lakini Facebook imeahidi kuwa siku za karibuni italeta App hiyo kupitia mfumo wa Android. Unaweza kudownload App hiyo kwa kubofya hapo chini na utapelekwa kwenye ukurasa maalum wa kudownload App hiyo kwenye soko la App Store.

Facebook Creator
Price: Free

Nini maon yako kuhusu App hii..? Tuambaie kwenye maoni hapo chini. Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha una download App ya Tanzania Tech kupitia Play Store pia usasahau kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech kupitia Youtube ili uweze kupata habari zote za teknolojia kwa njia ya Video.

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.