in

Hatimaye Tovuti ya ‘Zoom Tanzania’ Yaja na App ya Mfumo wa Android

Sasa unaweza kufanya yote kwa urahisi kupitia App ya Zoom Tanzania

zoom Tanzania Programu App

Zoom Tanzania‘ ni jina ambalo sio geni kwa hapa Tanzania, Vilevile kwa nje ya nchi Zoom Tanzania ni jina la tovuti inayofanya vizuri sana kwenye maswala mazima ya biashara za mtandaoni kwa maana ya kuuza na kununua pamoja na maswala mazima ya kusaidia muonekano wa biashara mbalimbali mtandaoni.

Kwa sasa mtandao wa Zoom Tanzania ni moja kati ya mitandao michache inayotegemewa sana na watanzania hasa kwenye maswala mazima ya ajira kwa maana ya kutafuta kazi pamoja na kutafuta wafanyakazi. Pamoja na mtandao huu kufanya vizuri kwa muda sasa hadi kufikia tarehe 16 mwezi huu kwa mara ya kwanza App ya Zoom Tanzania imeanza kupatikana kupitia mfumo wa Android.

Ikiwa ni moja kati ya hatua zilizo subiriwa kwa hamu na watanzania wengi sasa utaweza kufanya mambo ambayo ulikua unayafanya kupitia tovuti ya Zoom Tanzania kupitia App hiyo mpya ya mfumo wa Android.

App hiyo mpya ambayo sasa inakuja na sehemu mpya ya “Chat” inakupa uwezo mzuri zaidi wa kuwasiliana na wauzaji na wanunuzi wako kwa urahisi huku ikitumia kiasi kidogo cha Data kwa sababu ya kuwa na sehemu mpya ya “Data Mode”.

Apps Nzuri Kwa Simu za Android Zilizopo Rooted

Kwa kupitia sehemu hiyo mtumiaji ataweza kuchagua moja kati ya sehemu tatu ambapo kila sehemu itakupa uwezo tofauti wa kudhibiti Data pale unapotumia programu hiyo, vilevile programu hiyo itakupa uwezo wa kutengeneza “Alert” kama ilivyo kwenye tovuti yake pamoja na uwezo wa kuendesha matangazo yote na biashara yako moja kwa moja.

Unaweza kujaribu mwenyewe App hiyo kwa kupakua toleo hilo jipya la App ya Zoom Tanzania kwa kubofya hapo chini na utapelekwa moja kwa moja kwenye ukurasa wa App hiyo kwenye soko la Play Store kwa watumiaji wa Android.

ZoomTanzania
Price: Free

Kwa sasa bado hakuna taarifa zozote za App hii kutoka kwa mfumo wa iOS lakini pengine muda sio mrefu App hii itapatikana kwenye mfumo huo pia. Je umeonaje App hii mpya ya Zoom Tanzania..? tujulishe kupitia kwenye maoni hapo chini.

Kwa habari zaidi za Teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech nasi tutakujuza yote mapya kwa upande wa teknolojia, pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote kwa haraka zaidi.

Jaribu App Mpya ya Tanzania Tech Lite

Chanzo : Zoom Tanzania Blog

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.